Wednesday, December 21, 2016

AMPUNI YA SIMU YA TIGO YATAMBULISHA ZANA MPYA NA KUBORESHA ZANA YA TIGO PESA KWA WATUMIAJI WA SMARTPHONE

  Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kutambulisha zana mpya ya simu na kuboresha zana ya Tigo Pesa kwa watumiaji wa Smartphone. Kulia ni Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia.
 Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia (kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kazini.

 Na Dotto Mwaibale

 KAMPUNI  inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania  leo imezindua zana ya kipekee, ya kibunifu na sahihi  ambayo inatoa njia rahisi  ya kununua vifurushi vya tigo, kuboresha akaunti za wateja, kuangalia salio na muhimu zaidi  kujiweka katika mkondo wa matumizi ya data.

Kampuni hiyo pia imeboresha  zana yake ya Tigo Pesa kwa kuendelea kurahisisha njia ambazo wateja wake wanaweza kufanya miamala yao ya kifedha kwa njia ya simu.

Akielezea  zana hizo kwa vyombo vya habari  katika ofisi ya Tigo Jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore  alisema, “Zana zote za Tigo na Tigo Pesa ni ubunifu ambao unayafanya maisha kuwa rahisi na sahihi zaidi kwa wateja wetu. 

Wateja wetu wote wanaotaka kutumia zana hizo ni kiasi tu cha kuwa na kadi ya simu iliyosajiliwa, simu ya kisasa (smartphone) iliyo na iOS au inayoendeshwa na mifumo ya android. 

Kitu wanachotakiwa kukifanya ni kupakua zana kutoka katika jukwaa husika na kufuata maelekezo rahisi ya kuanza kutumia zana.  Hakuna haja ya kukumbuka  njia ya mkato ili kufanya muamala.  Halikadhalika ni njia nzuri sana  ya kudhibiti matumizi yako husuasni katika uhifadhi wa  data.”

Mpore aliongeza kuwa Tigo pia inazundua tena zana ya Tigo Pesa iliyoboreshwa ambayo itawawezesha watumiaji nchini kuzifikia pochi zao za Tigo Pesa  katika njia sahihi na rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa awali. Wateja wanweza kutuma  pesa  kutoka mtandao wowote, kilipia ankara (bili), kuhamishia benki, kuongeza salio na kutoa pesa vyote hivyo kwa ktumia  smartphone zao.

Akizungumzia  kuboreshwa kwa zana ya Tigo Pesa, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa tigo Raun Swanepoel  alisema, “Watumiaji wa Smartphone nchini wanweza kuendelea kufurahia  miamala yao ya Tigo Pesa kama kawaida  kwa kasi zaidi na kwa urahisi  kwa kutumia zana mpya iliyoboreshwa ya Tigo Pesa.”

Swanepoel aliongeza; “Hivi sasa unaweza kuangalia namba za mawasiliano ulizohifadhi katika simu yako unapochagua kutuma pesa kupitia  zana ya Tigo Pesa na hali kadhalika kuhifadhi  malipo yako ya kawaida pamoja na kuhamisha fedha kutoka benki kwa haraka hapo baadaye.”

Alisema kutambulishwa upya kwa zana hii  inayofahamika kama Tigo Pesa App mteja hatatozwa kwa data jambo ambalo ni sawa na ilivyo kwa Tigo App wakati unapingia katika utumiaji wa mtandao wa Tigo. 

Hali kadhalika wateja wanaweza kuzifikia kuzifikia pochi zao za tigo Pesa  wakiwa sehemu yoyote duniani  kupitia mtandao wa intaneti usiotumia nyaya Wi-Fi au  au data nyingine za simu zilizounganishwa ili mradi wawe na akaunti ya Tigo Pesa iliyosajiliwa.

 “Faida nyingine  ambayo imeletwa na zana hii kwa walio na akaunti ya fedha katika simu nchini  inawapa uwezo wa  wa kufikia kwa urahisi na kwa usahihi pochi moja  kwa kutumia zama kadhaa,” alihitimisha  mkuu huyo wa huduma za kifedha.




No comments: