Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara
Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao
WANANCHI halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa tena viwanja.
Wananchi wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.
Nestori Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.
Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.
Afisa ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka 2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.
Alisema kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.
Katika hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa amani bila bughuza.
Hata hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.
Alisema kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.
Hata hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi kushindwa kuvimiliki.
No comments:
Post a Comment