Sunday, December 25, 2016

WENGI WAJITOKEZA KWENYE MSIBA WA MPOKI BUKUKU TABATA

 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku

 Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na Shemeji wa marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.
 Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo
 Waandishi wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye alikuwa Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian
 Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo

 Mmmiliki wa Blogu hii, Kamanda Richard Mwaikenda, ambaye pia ni Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo, Kamanda Richard Mwaikenda (kulia) akiwa na wanahabari wenzie kwenye msiba huo.Kutoka kushoto ni Mpigapicha wa Waziri Mkuu, Hilary Bujiku, Mmiliki wa Blog ya K-VIS, Khalfan Said, Mmiliki wa Blog ya Michuzi, ambaye pia ni Mpiga Piacha na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Muhidini Issa Michuzi, Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, ambaye ni shemeji wa marehemu Mpoki, Edwin Mjwahuzi na Francis Chirwa ambaye ni mmoja wa viongozi wa Bodi ya Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema. ,

 Waombolezaji wakiwa kwenye msiba




Jirani rafiki wa karibu wa marehemu, Mpoki, maarufu kwa jina la Mijisu  akilia wakati wa msiba

No comments: