Monday, March 27, 2017

PPF YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA KITUO CHA AFYA LONGIDO



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto),
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango  wa PPF kwenye Jamii.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.
Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.
Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu aliungana na Bodi ya Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya  Afya 16 nchini vitakavyonufaika na  msaada wa vifaa hivyo.
Mhe. Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.
“Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, alisema, msaada wa vifaa hivyo ni moja ya majukumu ya Mfuko kusaidia jamii.(CSR), hivyo PPF itatoa msaada kama huo kwa hospitali na vituo vya afya vingine 15.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe.Daniel Chongolo, na  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw.Juma Mhina.

 Waziri Mhe. Mhagama akitoahotuba yake
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, (aliyesimama), akitoahotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, akitoa hotuba yake
Wakurugenzi wa PPF; Waliovaa suti kutoka kushoto, Mkurugenziwa Mifumo ya Kompyuta, Bw. Riobert Mtendamema, Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Martin Mmari, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw.Steven Alfred na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
 Mkuu wa Mkoawa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bi.Sara Barahomoka
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Aggrey Mlimuka, (katikati), Mjumbe wa Bodi Bi.Amelye Nyembe, (kushoto), na Mkurugebnzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Longido, Bw. Juma Mhina, wakiwa kwenye hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa PPF, Bi. Uphoo Swai, (katikati), akiwa na mwenyeji wa Longido wakifuatilia hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Martin Mmari
 Wakurugenzi na Mameneja wa PPF pamoja na watumishi wa Halmashauriya Wilaya ya Longido wakijumuika kwenye hafla hiyo
 Wananchi wa Longido walikuwa ni mashahidi wakati wa kupokea msaada huo
Mkurugenzi Mkuu wa PPF naujumbe wake wakipokewa na viongozi wa Kituo cha Afya Lungido walipowasili kukabidhi msaada huo

No comments: