Madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo la mererani pekee duniani yakiwa tayari yamekatwa na kusanifiwa sasa yatauzwa kimataifa katika kituo kitakachonjengwa Arusha |
Mtaalamu wa kukata madini Adam Idd Lacha akiwa anakata na kusanifu madini ya Tanzanite ya
kampuni ya Tanzanite one ambayo ndio inatoa mafunzo hayo. |
Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sky Associate Group, Faisal Juma Shahbhai akizungumza na madali wanawake wa madini |
Muonekano wa Mgodi wa kisasa wa uchimbaji madini wa tanzanite One Mererani kwa nje |
ANDREA NGOBOLE, PMT
Kampuni ya Tanzanite One, imetoa msaada
wa Sh 20 milioni kwa chama cha Madalali wanawake,wanaouza madini ya Tanzanite mkoani
Arusha .
Wakurugenzi wa kampuni hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja
na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO), Faisal Shabhai na Hussein Gonga walitangaza uamuzi
huo wakati wakizungumza na madalali , katika ukumbi wa polisi jijini hapa.
Faisal alisema kampuni yao ambayo inachimba Tanzanite, imetoa msaada wa sh 20 milioni,ili
kuendelea kutekeleza mahusiano mema na wadau wa Tanzanite na jamii ya wanawake
ambao wanajihusisha na biashara ya kuuza madini hayo.
Alisema msaada huo, umetokana na maombi ya
wanawake hao, kusaidiwa waliyotoa katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo na viongozi wa Tanzanite One.
Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetenga kiasi cha sh 200 milioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya
kisasa Mererani.
Gonga alisema kwa sasa tayari wametoa matofali
65,000 ambayo yapo eneo ambalo itajengwa hospitali hiyo ili kuondoa matatizo ya
ukosefu huduma za afya katika mji wa Mererani.
Awali Mwenyekiti wa chama hicho, Eugen
Augustine alisema madalali wa madini wanawake mkoani Arusha, wanakabiliwa na
tatizo la mtaji mdogo na hivyo kushindwa kunufaika na biashara yao.
Alisema kutokana na tatizo hilo, ndio sababu
waliomba msaada kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha na Tanzanite One ili wasaidiwe.
Katika hatua nyingine, Kampuni hiyo, imetoa
msaada wa mahindi magunia 250 kwa
wananchi wakazi wa kata ya Naisinyai ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo
kwa jamii inayozunguka migodi yake.
Faisal alisema msaada huo, utasaidia makundi
maalum katika jamii na ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kushauri kampuni hiyo, iongeze misaada kwa jamii inayowazunguka.
Kampuni ya Tanzanite One inamilikiwa kwa pamoja
na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO).
No comments:
Post a Comment