Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wiki iliyopita, wakati wa uzinduzi wa bima ya afya hapa nchini. Katikati
ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson. (NA MPIGA PICHA WETU)
ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson. (NA MPIGA PICHA WETU)
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).
Bima hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5 mpaka milioni 200.
Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi (ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.
Pia bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za eksirei na uchunguzi wa kimaabara.
"Bidhaa hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao" alisema Lokonyo.
Lokonyo alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.
Uzinduzi wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.
"Bima hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.
Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.
Kampuni ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na benki.
No comments:
Post a Comment