Sunday, June 4, 2017

MBUNGE AWESO ATAJA SABABU YA WILAYA YA PANGANI KURUDI NYUMA KIUCHUMI


MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ametaja sababu kubwa iliyoifanya wilaya hiyo kurudi nyuma kiuchumi ni kutokana na kuchelewa kuwekeza kwenye suala la elimu na miundombinu ya barabara ambacho ni kilio cha muda mrefu.

Hivyo kuitaka jamii kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye elimu ili iwe chachu ya

kuinua maendeleo yao lakini pia serikali iboreshe miundombinu ya barabara ya Tanga -Pangani hadi Sadaani ambayo imekuwa ikipigiwa kelele na wabunge waliopita bila mafanikio

Aweso aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo ambapo alisema wazazi hawana budi kuwekeza kwenye elimu iliwaweze kupatikana wataalamu watakaosaidia harakati za kuinua maendeleo.

Alisema ili katika mipango mikubwa ya kufanikisha azma hiyo ndio sababu kubwa wakaanzisha mpango mahususi wa niache nisome mwaka jana ambao umepata mafanikio makubwa.

“Mpango wa niache nisome umekuwa mkombozi mkubwa wa kuihamasisha jamii ya wana pangani kuona umuhimu wa kupata elimu na mafanikio yaliyopatikana ni mengi ikiwemo kupata fursa mwaka huu kuwapeleka vijana wengi Jeshini “Alisema

Aidha aliwataka viongozi chama na serikali kuendelea kushirikiana na wataalamu ili kuwezesha kuifungua wilaya ya Pangani ambayo inahitaji kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Uchumi wa Pangani ni zao la Mnazi na mtu mpaka aje wilayani hapa lazima awe na sababu maalumu ikiwemo kufiwa nah ii inasababishwa na miundombinu mibovu ya barabara hivyo ujenzi huo utakapoanza utasaidia kufungua uchumi huo “Alisema.

Mbunge huyo aliwataka pia wananchi wa wilaya hiyo kutunza maeneo yao kwa kuacha kuyauza ovyo kutokana na fursa kubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta.

 Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments: