Wednesday, July 5, 2017

MAONESHO YA SABASABA 2017: HUDUMA ZA PSPF NI "CHAP CHAP", AFISA WA POLISI ASEMA


Modesta Mchopa wa PSPF, (kulia), akimpatia taarifa za michango mwanachama wa Mfuko huo, Afisa wa polisi, E.M Peter, aliyefika kwenye banda la Mfuko huo leo Julai 5, 2017. Afisa huyo wa polisi amesifu utoaji huduma wa wafanyaakzi wa Mfuko huo ambapo alisema yeye ametumia sekunde 30 kupatiwa taarifa yake.(NA K-VIS BLOG/Khalfan Said)
 Mhandisi mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Ally R. Shanjirwa (kulia), akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa
Mfuko huo, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Bi.Julieth Mwiziko, punde tu baada ya kujiunga.
Afisa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Irine J. Musetti(kulia),
akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Bi.Sakina Iddi Tundu, punde tu baada ya kujiunga.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi (kulia), akimsaidia mama huyu kujaza fomu za kujiunga na PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari PSS.


 Mwanachama huyu akiwa amepatiwa taarifa za michango yake papo hapo
 Mwanachama akisoma taarifa za michango yake
 Binti huyu akisoma kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za PSPF
Bi. Modesta Mchopa, ambaye naye ni afisa wa PSPF aliye kwenye mafunzo. akiwahudumia wanachama hawa wa Mfuko huo waliofika kujua michango yao.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), akimwelekeza jambo Mfanyakazi wa PSPF aliye kwenye mafunzo ya vitendo, Bw.Honorath Tillya, (watatu kushoto), huku mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko huo (kulia), akijaza kitabu cha wageni. Wakwanza kushoto ni Modesta Mchopa, ambaye naye ni afisa wa PSPF aliye kwenye mafunzo.
Win-God, (kushoto), Afisa wa uendeshaji msaidizi wa PSPF, waliwahudumia wateja.
Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF anayeshughulikia masuala ya uchangiaji wa hiari (PSS), Bi. Asmahan H. Haji,(kulua), akiwahudumia wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo.
 Anna Lukando, katikati anayeangalia camera), ambaye ni Afisa Mipango wa Taasisi ya Ardhi Plan Limited,  ambayo ni mshirika wa PSPF katika masuala ya  viwanja, akiwapatia maelezo wananchi waliofika banda la PSPF ili kupatiwa huduma za uanachama. Wanachama wa PSPF kwa mujibu wa sheria, wanaweza kukopeshwa viwanja na taasisi hiyo.
 Anna Lukando, (kushoto), ambaye ni Afisa Mipango wa Taasisi ya Ardhi Plan Limited,  ambayo ni mshirika wa PSPF katika masuala ya  viwanja, akiwapatia maelezo wananchi waliofika banda la PSPF ili kupatiwa huduma za uanachama. Wanachama wa PSPF kwa mujibu wa sheria, wanaweza kukopeshwa viwanja na taasisi hiyo.
 Afisa Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA), wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Mariam Ibrahim, (kulia), akiangalia jinsi mwananchi huyu anavyojaza fomu ya kujiunga na Mfuko huo kupitia uchangiaji wa Hiari, (PSS), kwenye banda la PSPF lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama (sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam ambako kunafanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Afisa msaidizi mwendeshaji wa PSPF, Bw. Musa Mfaki, (kulia), akimuhudumia mwananchi
Bw. Isack Kimaro, (kushoto), Afisa wa uendeshaji PSPF, akimuhudumia mwananchi aliyejiunga kwenye mpango wa PSS
Afisa wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), aliye kwenye banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Imani Masebu, (wapili kulia), akiwafafanulia masuala muhimu yahusuyo hifadhi ya jamii wananchi hawa waliofika wkenye banda la Mfuko huo. Kulia ni Afisa Mkuu wa Mifumo ya Kompyuta wa PSPF, Bi. Mariam Ibrahim.
Kikao cha tathmini ya kazi iliyofanyika kutwa nzima katika banda la PSPF kikiongozwa na mkuu wa timu inayoshiriki kuwahudumia wananchi kwenye banda hilo Bw. Abdul Njaidi.

No comments: