Mwenyekiti wa kamati ya harusi (kushoto) na katibu wake.
Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya waliookoka katika kanisa hilo huku tayari wakiwa wanaishi na wenza wao kama mme na mke bila kufunga ndoa takatifu, wamepata fursa ya kufungishwa rasmi ndoa takatifu. Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema si vyema waliookoa kuishi kama mme na mke huku wakiwa hawajafunga ndoa takatifu madhabahuni mwa Bwana hivyo jumapili ijayo Julai 16,2017 zitafungwa ndoa za pamoja zaidi ya tisa kwa waumini waliookoka huku tayari wako kwenye ndoa bubu.
"Usikae na mme au mke bila kufunga ndoa, maana ndoa bubu itakukotea puani. Acha kuvaa mapete ya ajabu ajabu bila kufunga ndoa. Unakuta lipete lina kichwa cha nyoka, jiulize hilo lipete umepewa na nani? Huenda ndiyo maana unaandamwa na mapepo". Alisisitiza Dkt.Mchungaji Kulola. Baadhi ya wanaotarajiwa kufunga ndoa siku hiyo, wamefurahishwa na fursa waliyoipata huku wakisema aina hiyo ya ndoa ni nzuri kwa kuwa hawatatumia gharama kubwa kwani baada ya kufunga ndoa, watapata chakula cha pamoja kanisani hapo na baadaye kurejea nyumbani. Tukio hilo la kihistoria litaanza saa nane kamili mchana katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza na watu wote wanakaribishwa kulishuhudia ambapo baada ya ndoa hizo kufungwa, itafanyika tafrija fupi kanisani hapo ambapo watu watakula na kunywa pamoja na wanandoa hao.
No comments:
Post a Comment