Mgeni Rasmi- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha. Picha zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki sala ya kumuombea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Wanachama wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA) wakifatilia Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping
Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017. Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro akitoa salamu za Mkoa muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mkazi wa Moshi Mkoani Kilimanjaro ambaye ni Mwanachama wa TFA Shekh Ally Mwamba akiongoza wanachama wa TFA kumuombea Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya
Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA). leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na Katibu wa Kampuni ya TFA na Ofisi ya kisheria Bi Pendo Jacob mara baada ya
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA), Mwingine ni Bi Cathy Elizabeth S. Long'lway. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mgeni
Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu Kazi za TFA banda la TFA mara baada ya
ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA), Kulia kwake ni Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, na kushoto kwake ni Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro. leo Octoba 28, 2017 Jijini Arusha.
Mwanachama wa Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) Bi Mwanahamisi Salim Bakari akitoa shukrani zake kwa Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.
Picha ya pamoja Mgeni Rasmi-Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb), Mwenyekiti wa TFA Ndg Peter Ezrah Sirikikwa, Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Arusha Mhe Gabriel Fabian Daqarro na viongozi wengine wa TFA mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping
Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha, leo Octoba 28, 2017.
Na Mathias Canal, Arusha
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe
Dkt Mary Mwanjelwa (Mb) leo Octoba 28, 2017 amekipongeza Chama cha Wakulima wa
Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kufungua matawi mengi nchini ya kuuza pembejeo
bora za kilimo.
Mhe Mwanjelwa ametoa
pongezi hizo wakati akihutubia kwenye Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wanachama wa
Tanganyika Farmers’ association (TFA) uliofanyika katika ukumbi wa TFA Shooping
Centre, Ngarenaro – Jijini Arusha.
Alisema kuwa hiyo ni
ishara njema ya kuunga mkono Ilani ya Chama cha Mapinduzi na juhudi za Serikali
katika kuendeleza Sekta za kiuchumi ambazo ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alisema kuwa Kwa wajibu
huo, Wizara ya kilimo imeona juhudi kubwa na za makusudi za Kampuni ya TFA jinsi ilivyojipanga katika
kuwahudumia Wananchi na Wakulima nchini.
Kupitia Mkutano huo
Aliwaomba Wananchi wote kuendelea kuiunga mkono Kampuni ya TFA ili waweze
kupata maendeleo ya haraka kwa kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo
ili kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo cha kisasa.
Mheshimiwa Dkt Mwanjelwa
alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli imetoa msukumo mkubwa katika
kuendeleza Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na hasa kwa kuzingatia kuwa nchi imeaanza safari ya
kuelekea kwenye uchumi wa Viwanda ambao unazitegemea Sekta hizo kama chanzo cha
malighafi kwa ajili ya kuziongeza thamani bidhaa lakini pia kuzisindika kwa
ajili ya biashara katika soko la ndani na nje.
Alitoa Rai kwa Wananchi
wote na Wanachama wa TFA kutumia vizuri mtandao wa Mawakala wa TFA, kwani
inalenga kumuondolea Mkulima matatizo ya upatikanaji na matumizi ya pembejeo
hafifu za kilimo.
Alisema hiyo ndiyo ishara
ya kuifanya TFA iweze kuendelea kutoa huduma zake kwa kipindi chote cha zaidi
ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwake.
“Nichukue fursa hii nafasi
hii kuwakumbusha wanachama wa TFA na Wananchi kwa ujumla kuwa, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amedhamiria kuendeleza Viwanda vilivyopo
hapa nchini, na kuanziasha vipya, nanyi kama Wabia, Wadau wa Wakulima katika
kuchangia maendeleo ya viwanda hivyo, natoa rai kwenu kuendelea kukithamini
kilimo kwa kuongeza tija na uzalishaji, ili viwanda vilivyopo na
vitakavyoanzishwa viweze kupata malighafi na rasilimali zakutosha na hatimaye
tufikie kwenye uchumi wa kati” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa alisema
kuwa Wizara ya Kilimo imeamua kuweka utaratibu wa kununua mbolea hapa nchini
kupitia Mfumo wa Ununuaji wa Pamoja ya “Bulk Procurement System - BPS” na
wakati huohuo kuanzisha Mfumo wa Kuuza Mbolea kwa bei Elekezi, ambapo kwa
sehemu kubwa ya nchi mbolea imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.
Mfumo huo unalenga
kupunguza kero ya upatikanaji na ulanguzi katika bei za mbolea. Kupitia mfumo
huo, Serikali inaamini matumizi ya mbolea hapa nchini yataongezeka kwa kiasi
kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita, na kuwa na ongezeko kubwa la
uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Huduma zinazotolewa na TFA
ni kuuza Zana bora za kilimo, Pembejeo za kilimo kama Mbolea, Mbegu bora,
Viuwatilifu mbalimbali pamoja na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa
Wakulima, kama juhudi ya kumpunguzia mkulima, mmekuwa mkiagiza baadhi ya
pembejeo toka nje ya nchi kwa kuzingatia sheria na taratibu zote. Nawapongeza kwa jinsi mlivyojipanga vema
katika kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuleta
mabadiliko makubwa katika Sekta ya Kilimo.
Katika Mkutano huo hoja mbalimbali zimeibuka kutoka kwa wanachama ikiwemo Ongezeko la gharama za mahindi katika Mkoa wa Njombe hoja ambayo Mhe Naibu Waziri ameahidi kuzuru Mkoani Mbeya kufatilia jambo hilo.
Aidha, Baadhi ya wanachama wamempongeza Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli kwa kufuta
Jumla ya tozo 80 ambapo kati ya tozo 139 zimefutwa na
tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha kufutwa
kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.
Kwenye zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari
zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo mbili
zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).
Katika kuongeza
upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango
kwenye mbolea na tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa.
Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment