Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles John Tizeba
Viongozi wa serikali, Taasisi binafsi, Wadau wa
kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wananchi kwa ujumla wake wameombwa kushiriki kikamilifu
katika Maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Katika
VIwanja vya CCM Kalangalala Mkoani Geita.
Msisitizo huo umejikita zaidi kwa wananchi wote
ambapo umuhimu zaidi umeelekezwa Kwa wakazi wa Mkoa wa Geita na
mikoa jirani ukiwemo mkoa wa Mwanza, na Kagera ili kujionea Maonyesho ya kazi mbalimbali zinazolenga kuongeza uzalishaji, tija na upatikanaji wa chakula na usindikaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
mikoa jirani ukiwemo mkoa wa Mwanza, na Kagera ili kujionea Maonyesho ya kazi mbalimbali zinazolenga kuongeza uzalishaji, tija na upatikanaji wa chakula na usindikaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Kusikiliza Nyimbo, ngonjera, mashairi na ngoma za
asili zinazohamasisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula sambamba na Kupata
elimu juu ya hifadhi ya mazingira – udongo, maji na viumbe hai.
Akizungumza na waandidhi wa habari Ofisini kwake
Jijini Dar es salaam Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles John Tizeba alisema kuwa
maadhimisho hayo ya wiki ya chakula ambayo hufanyika kuanzi Octoba 10 mpaka
Octoba 16 kila mwaka huwa na dhamira ya Kuwawezesha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi
kujifunza teknolojia sahihi za kuongeza uzalishaji na tija katika Sekta za Kilimo,
Mifugo na Uvuvi kwa lengo la kupata chakula bora na cha kutosha kwa kila mtu na
kwa wakati wote.
Alisema ni njia mojawapo kwa wakulima kupata
utambuzi wa Kuongeza jitihada na mbinu za kutokomeza njaa, utapiamlo na
hatimaye kuondoa umaskini, Kufahamu mikakati thabiti inayoainishwa ya
kuhakikisha kila mtu anapata chakula bora na cha kutosha wakati wote, na Wataalamu
mbalimbali wa kilimo kuwaelimissha Wananchi ili kuondokana na mila potofu
zinazozuia baadhi ya jamii kula aina fulani za vyakula, kwa mfano kutokula
mayai kwa akina mama wajawazito.
Dkt Tizeba alizitaja faida zingine za maonesho
hayo kuwa ni pamoja na Kuimarisha Ushirikiano wa Kitaifa na Kimataifa katika
masuala ya kukuza na kuendeleza kilimo, ufugaji na uvuvi, ikiwa ni pamoja na Kuelezea
kihistoria, nafasi ya mila na utamaduni katika kuendeleza sekta za kilimo,
ufugaji na uvuvi kwa lengo la kuongeza tija na uzalishaji.
Alisema kuwa Kila mwaka Makao Makuu ya FAO
huchagua Kaulimbiu ambayo huwa ndiyo dira ya kuhamasisha wadau wote wa sekta ya
kilimo kuchangia katika kuhakikisha kila mtu anawezeshwa kupata chakula bora na
cha kutosha wakati wote wa maisha yake.
Kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Badili
mwelekeo wa uhamaji; Wekeza katika usalama wa chakula na maendeleo Vijijini”.
Kaulimbiu hii
inaweka umuhimu katika kuweka Mipango na Programu zinazolenga kuongeza tija na
uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo Vijijini; kupuza utegemezi na kuongeza
usawa katika Jamii, sambamba na uhifadhi mazingira ambayo ndiyo muhimu katika
maendeleo ya kilimo na hifadhi ya Jamii ili yachochee jitihada za kuondoa
umaskini kwa kutumia nguvukazi ya Rasilimali Watu hususani Vijana ambayo imekuwa ikihamia Mijini kwa
lengo la kujitafutia mahitaji ya muhimu na mazingira bora.
Chimbuko
la Siku ya chakula ni Mkutano wa mwaka 1979 ambapo nchi wanachama wa FAO
zilikutana Jijini Quebec nchini Canada na kujadili kiundani masuala mbalimbali
kuhusu chakula. Mojawapo ya maazimio ya mkutano huo ilikuwa kutenga siku moja
ya kila mwaka ili kuzungumzia na kutafakari njia na mbinu mbalimbali za kupata
chakula cha kutosha kwa watu wote duniani na kwa wakati wote.
Maadhimisho ya kwanza ya siku hii yalianza mwaka
1981. Hivyo maadhimisho ya mwaka huu ni ya 36 na yanasherehekewa kwa pamoja na
maadhimisho ya miaka 72 ya kuanzishwa
kwa FAO tarehe 16 Oktoba, 1945.
MWISHO
No comments:
Post a Comment