Saturday, October 21, 2017

MKIKITA WAMLAKI KWA SHANGWE MFILIPINO MTAALAMU WA MASOKO

 Mtaalamu wa masuala ya Masoko kutoka Ufilipino, Dk.Wenfredo Muni akikabidhiwa zawadi ya maua na Meneja Uhusiano wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Neema Fredrick
wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam  jioni hii. Aliyevaa fulana ya njano ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange na Mdau Haji Mohamed. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Dk Muni akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mkikita, Elizabeth akimsalimia Dk. Muni
 Waziri wa zamani wa Afya, Dk. Rashid Seif akisalimiana na Dk. Muni
 Dk. Rashid Seif akikumbatiana kwa fura na Dk. Muni wakati wa mapokezi
 D. MUni akifurahia zawadi ya shada la maua
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mkikita, Dk. Kissui S Kissui akisalimiana na Dk. Muni wakati wa kumlaki mgeni huyo kutoka ufilipino
 Mdau Suchekk Bangragh ( wa pili kulia akimlaki kwa furaha Dk Muni
 Wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Dk. Muni
 Dk. Muni huyoooooooo
 Wakiangalia pasi ya kusafiria ya Dk Muni

Wakiondoka Uwanja wa Ndege


Na Richard Mwaikenda

UONGOZI  wa Mtandao wa Kijani 

Kibichi Tanzania (Mkikita), ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Kisusui S Kissui   na Mkurugenzi Mtendaji, Adam Ngamange kumlaki Mtaalamu wa Masoko kutoka Ufilipino,  Dk.Wenifredo Muni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mtalaamu huyo ambaye atakuwa nchini kwa miezi mitatu kwa mualiko wa Mkikita atafanya semina mbalimbali pamoja na kutembelea mashamba yanayosimamiwa na matandao huo yakiwemo pia ya watu binafsi blia kusahau mifugo.

Akizungmza wakati wa mapokezi, Mkurugenzi wa Mkikita, Adam Ngamange amesema kuwa ujio wa mtalaamu huyo utawanufaisha wakulima na wafugaji wa mtandao huo kwa kupanua uwanja mpana wa masoko ya mazao na mifugo nje ya nchi.

Aliwaasa wanachama kutoiacha fursa hiyo pekee ambayo haijawahi tokea na kuwataka kuhudhuria semina zilizoandaliwa ili wapate matokeo chanya ya fursa za masoko duniani.

Katika mapokezi hayo Mkikita iliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dk. Kissui S Kissui, Wajumbe wa Bodi, Catherina Edward, Neema Fredrick na Elizabeth na baadhi ya wanachama wa mtandao huo.

Wadau wengine waliojitokeza kumpokea ni aliyekuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Rashid Seif., Haji Mohamed, Suchekk Bangragh na Mbaga Edward.



No comments: