Afisa Metekelezo wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha,Miraji Kisile akiwahamasisha
wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma
zinazotolewa ikiwemo za matibabu
Afisa Metekelezo wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Arusha,Miraji Kisile
akiwahamasisha
wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma
zinazotolewa ikiwemo za matibabu
zinazotolewa ikiwemo za matibabu
ELIMU ikiendelea kwenye moja ya
masoko Jijini Arusha kuhusu umuhimu wa wajasiriamali kujiunga na mfuko
huo ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za
matibabu
MFUKO wa Taifa wa Bima ya
Afya Mkoani Arusha (NHIF)
umeanza
kutoa elimu ya bima ya afya mtaa kwa mtaa kwa wakazi wa mkoa huo ili waweze
kujiunga nao ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za
matibabu.
Hayo yalibainishwa na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya Mkoani Arusha ,Miraji Kisile
ambapo alisema lengo ni kuhamasisha wazazi na walezi kuwaandikisha
watoto wao na mpango wa toto afya kadi kwa chini ya miaka
18.
Alisema mfuko huo umeamua kushiriki katika zoezi hilo
kikamilifu kwa kupita katika masoko na magulio ambayo asilimia kubwa ya
wananchi wamekuwa wakipatikana huko.
Aidha alisema sambamba na hilo lakini pia uongozi wa
mfuko huo wamedhamiria kuwahamasisha wajasiriamali mbalimbali kujiunga na mfuko
huo kupitia mpango wa kikoa ili kulinda mitaji yao kwa kuwa na uhakika wa
huduma za afya na matibabu kupitia NHIF kwa gharama
nafuu.
“Zoezi hilo limeanza Octoba 18 mwaka huu na litafanyika
kikamilifu kwa muda wa miezi miwili lengo ni kuwafikia wakazi wengi wa mkoa wa
Arusha na viunga vyake “Alisema.
Alisema kwa sasa mfuko huo unatoa kipaumbele kusajili
watoto kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwa gharama za kitanzania 50400 kwa
mwaka ambapo ataweza
kuhudumiwa kwa
vituo 7000 vilivyosajiliwa na bima ya afya vikiwemo hospitali zote za
serikali,Hospitali zinazomilikiwa na Madhehebu ya dini,Hospitali za watu
binafsi, maduka ya dawa pamoja na vituo maalumu vya
uchunguzi.
Zoezi hilo limefanyika na kutarajiwa kuendelea kufanyika
kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Tengeru,Soko la Ngaramtoni,Soko
Kuu,Soko la Kilombero,Soko la Mbauda,Soko la Namanga, Mnadani
Monduli,Loliondo,Digodigo Ngorongoro na Waso
Ngorongoro.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments:
Post a Comment