Binagi Media Group
Shirika la kutetea
haki za wasichana na wanawake, Hakizetu lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini
Mwanza, limezindua mradi ujulikanao kama “Kila Mtu Aishi Vyema Kuanzia Sasa”
awamu ya pili (Living Better Today Project
phase II), lengo ikiwa ni kutokomeza ukatili katika jamii.
Mradi huo
umelenga kufanya kazi katika Kata mbili za Ibungiro na Nyamanoro katika
Manispaa ya Ilemela ambapo vikundi mbalimbali vya kijamii vitaundwa hadi katika
ngazi ya jamii na wanafunzi
wa sekondari katika shule za Mwanza Baptis na Ibungiro na kujengewa uwezo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa elimu ya kujikinga na ukatili wa kijinsia katika jamii.
wa sekondari katika shule za Mwanza Baptis na Ibungiro na kujengewa uwezo kwa ajili ya kusaidia utoaji wa elimu ya kujikinga na ukatili wa kijinsia katika jamii.
Akizungumza jana
kwenye uzinduzi wa mradi huo, Afisa Miradi wa shirika la Hakizetu, Gervas Evodius alisema awamu ya kwanza ya mradi huo
iliwafikia wananchi 2,400 katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana hivyo awamu ya
pili matarajio ni kuwafikia wananchi 300 ambao watakuwa mabalozi wa kutoa elimu
ya kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii.
Alisema
mradi umelenga kufanya kazi zaidi katika ngazi za jamii/ familia ambapo kuna
mzizi wa ukatili kwa wasichana na wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni na
kwamba matarajio ni kutatua changamoto hiyo katika jamii.
Evodius
alisema ni wakati mwafaka kwa wanajamii kuungana pamoja ili kutokomeza ndoa na
mimba za utotoni pamoja kila aina ya ukatili wanaokumbana nao wasichana na
wanawake kwani ni jukumu la kila mmoja kuwakinga.
Mkurugenzi
wa shirika hilo, Cunegunda Ngereja alisema shirika linatoa elimu pamoja na
kuwawezesha kiuchumi wahanga wa ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo
kuwawezesha kiujasiriamli ili kuondokana na umaskini kwani umaskini na ukatili
katika jamii huchangia mimba na ndoa za utotoni.
Alisema
wanashirikiana na wadau mbalimbali kupitia vikao na kuweka mikakati ya pamoja
ya kuhakikisha mtoto wa kike na wanamke wanakua salama katika jamii.
Mmoja wa
washiriki wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Mwanasheria Akram Salim, alisema
wanajamii wanapaswa kuelewa kwamba ukatili wa kijinsia katika jamii umepitwa na
wakati hivyo ni vyema kuwa na mtazamo chanya wa kutambua kuwa kujihusisha na ukatili
wa kijinsia ni kuvunja sheria za nchi.
Naye Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mkudi katika Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela, Salum Heri alisema
baadhi ya watoto wa kike hukumbana na ukatili wakiwa nyumbani ikiwa ni pamoja
mbimba za utotoni kutoka kwa watu wa karibu na hivyo sheria kushindwa kuchukua
mkondo wake kutokana na kesi za aina hiyo kumalizwa kifamilia ambapo alitoa rai
kwa shirika la Hakizetu kuendelea kuwasaidia kielimu na kiujasiriamli wasichana
waliokumbana na ukatili wa aina hiyo ili kuwaondoa kwenye utegemezi katika
jamii.
No comments:
Post a Comment