Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano
uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,
Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano
uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
akifatilia mada kuhusu Mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja na wahariri wa
vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo
Novemba 24, 2017.
Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi-Naibu waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Leo Novemba 24, 2017.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Wanahabari kote nchini wametakiwa kutoa ushirikiano kwa
Wizara ya Kilimo ili ifanikiwe katika jitihada zake za kuhakikisha kwamba
Tanzania inafikia lengo la Azimio la Maputo la kumwezesha
mkulima kufikia matumizi ya kilo 50 za virutubisho kwa hekta badala ya hali ya
sasa ambapo anatumia kilo 19 tu au asilimia 38 ya lengo la Maputo.
Mwito huo umetolewa Leo Novemba 24, 2017 na Naibu waziri
wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati akizungumza na wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari nchini kwenye Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa
mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mkutano huo ulikuwa na dhamira ya kujifunza na kuongeza uelewa kwa wahariri juu ya Mifumo
mipya iliyoanzishwa na Serikali kuhusu Uagizaji wa Mbolea kwa Pamoja (Bulk
Procurement System - BPS) na Usimamizi wa bei Elekezi ya Mbolea (Indicative
Pricing Structure - IPS) kwa lengo la kumwezesha Mkulima kupata mbolea
bora na kwa bei nafuu ili kuongeza matumizi ya mbolea yatakayo chochea,
ongezeko la uzalishaji nchini ili kukidhi mahitaji ya familia na kuuza ziada
ndani na nje ya nchi.
Mhe Mwanjelwa alisema Wizara ya Kilimo
imebaini kuwa wafanyabiashara wadogo wa mbolea wanaokiuka bei elekezi kutokana
na wafanyabiashara wakubwa kuwauzia wafanyabiashara hao wadogo kwa bei elekezi
ya rejereja badala ya bei ya jumla licha ya kufahamu kuwa wanatakiwa kugawana
faida na wauzaji wa rejareja lakini bado wanakiuka taratibu za kisheria hivyo
aliwasihi kuacha tabia hiyo ili mawakala wauze kwa rejareja na kwa bei elekezi
bila kuathiri biashara zao.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ina Mkakati wa
kuongeza matumizi ya mbolea ambao umekuwa na umuhimu wa pekee hasa ikizingatiwa
kwamba imeweka lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati
unaoendeshwa kwa viwanda.
Alisema Kwa sehemu kubwa, viwanda hivyo vitategemea
malighafi itokanayo na mazao ya kilimo. Hivyo ili, kufikia lengo hilo, lazima
kila mmoja kutumia nafasi yake kuhakikisha kwamba tija itokanayo na Kilimo
inaongezeka kwani Mbolea ni moja ya vichocheo vikubwa.
“Pamekuwepo na Mifumo mbalimbali iliyoanzishwa kwa lengo
la kumsaidia Mkulima kupata mbolea za
kutosha ili aongeze tija na uzalishaji katika kilimo ambayo ni pamoja na ruzuku
ya usafirishaji ili kuwezesha mbolea kuuzwa kwa bei moja nchi nzima (Pan Territorial Prices). Baadae
ulifuata Mfumo wa wauzaji kulipwa sehemu ya bei na hivyo mbolea kuuzwa kwa bei
chini kuliko bei ya Soko. Sambamba na Mfumo huo, kulikuwa na jitihada za
kutengeneza mbolea hapa nchini ili kuepuka gharama kubwa za uagizaji”
Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Alisema taarifa zinabainisha kuwa Mikoa ya Ruvuma, Lindi,
Mtwara, Mwanza na Geita wafanyabiashara hufungua mifuko na kuuza mbolea ya
kupandia (DAP) kwa Tshs 2,000/= kwa kilo ili wapate Tshs 100,000/= kwa mfuko wa
kilo 50 badala ya bei elekezi ya Tshs 51,000 – 56,000/=.
Aidha, Mbolea ya kukuzia (Urea) wanaiuza kwa Tshs 1,500/=
kwa kilo ili wapate Tshs 75,000/= kwa mfuko wa kilo 50 badala ya bei elekezi ya
Tshs 41,000 – 45,000/=. Pamoja na kuwauzia wakulima mbolea iliyopoteza ubora
kwa kufunguliwa na kuachwa wazi, wafanyabiashara hawa wanawaingizia wakulima
hasara kubwa ya mavuno.
Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa alisisitiza, “Ofisi yangu ina
taarifa kwamba baadhi ya wafanyabiashara wanatunza mbolea bila kuzingatia
viwango vilivyowekwa na TFRA. Haya ni makosa mabubwa sana kisheria kwani
yanasababisha mbolea kumfikia mkulima ikiwa imepungua ubora au kuharibika
kabisa na hivyo kumfanya mkulima asipate tija inayotokana na matumizi ya
mbolea. Huu ni uhujumu mkubwa sana wa uchumi wa Mkulima pamoja na Taifa kwa
ujumla”
Mbolea ni kemikali ambayo virutubisho vyake huyeyukia
hewani ikiachwa wazi kwa muda mrefu. Kwa maana nyingine, kitendo cha kufungua
mfuko wa mbolea hufanya virutubisho (Nutrients)
kuanza kupotea mara tu vinapokutana na hewa. Hivyo kinachobaki kwenye mfuko ni
makapi yasiyo na manufaa katika kuongeza uzalishaji wa mazao. Aidha, mbolea ya
kupima inaweza ikageuka sumu kwa mimea na hata udongo na hivyo kufanya usifae
tena kwa matumizi ya kilimo.
Mkutano huo wa Naibu Waziri wa Kilimo na wahariri wa
vyombo vya habari nchini ni mwanzo wa mahusiano chanya baina ya Waandishi wa
habari na Wizara ya kilimo ili kuinua sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuunga
mkono kwa vitendo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt
John Pombe Magufuli katika kuimarisha uuchumi wa Wananchi kupitia kilimo ambao
ni uti wa mgongo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment