MWILI uliofukuliwa hivi karibuni kwa
kibali cha mahakama kuondoa utata wa taarifa za kupotea kwa Mwanafunzi wa
kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Scolastica, Humphrey Shayo (16) utazikwa
kwa mara ya pili leo (Jumamosi ) .
Hatua ya kuzikwa kwa mwili huo
uliokaa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa zaidi
ya siku 14
sasa inatokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Shayo.
sasa inatokana na kutoka kwa majibu ya sampuli ya vina saba (DNA) ikionyesha kuwa mwili ni wa Humphrey Shayo.
Kwa mujibu wa baba mzazi wa marehemu
Humphrey,Bw Jackson Makundi alisema mazishi yatafanyika katika kijiji cha Mamba
kwa Makundi ,Marangu wilaya ya Moshi baada ya kupata kibali cha mahakama cha
kuruhusu kuzikwa kwa mwili huo.
Makundi alisema shughuli za mazishi
ya mwanae yataoongozwa na maaskofu wasaidizi kutoka Dayosisi ya Dodoma akiwemo mchungaji
Samwel Mshana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) wakisaidiana
na Askofu Msaidizi wa (KKKT) dayosisi ya Kaskazini Mchungaji Elingaya Saria.
Novemba 6,mwaka huu taarifa za
kutoweka kwa mwanafunzi huyo katika shule aliyokuwa akisoma ya Scolastica
iliyopo mji mdogo wa Himo zilianza kuzagaa katika mitandao ya kijamii na baadae
Novemba 7 mwaka huu mwili ulikutwa ukiwa umetelekezwa mto Ghona unaokadiliwa
kuwa mita 300 kutoka katika shule hiyo.
Mwili huo ambao awali ulifikishwa
katika Hosptali ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ulipokelewa na kuhifadhiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti na baadae kuzikwa na Halmashauri ya Manispaa
ya Moshi katika makaburi ya Karanga kama
mwili usiokuwa na ndugu.
Hata hivyo,baada ya kuwepo kwa
taarifa ya kuzikwa kwa mwili huo ,familia ya Makundi iliomba kibali cha
mahakama kuruhusu kufukuliwa mwili huo
kwa lengo la kujiridhisha ,mtu aliyezikwa kama kweli ni mzee kama taarifa za
awali zilivyotolewa au ni ndugu yao.
Tayari watuhumiwa watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la
Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi huyo wamefikishwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji .
Waliofikishwa mahakamani ni pamoja
na anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo , aliyekuwa
mlinzi wa shule hiyo Hamis Chacha na Labani Nabiswa raia wa Kenya anayetajwa
kuwa Mwalimu katika shule hiyo.
Mbele ya mahakama ya Hakimu mkazi
,Moshi ,upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi
,Julieti Mawore uliwakilishwa na Mwanasheria wa serikali Kassim Nassiri
akisaidiana na Wakili wa kujitegemea ,Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi
ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili katika
shtaka hilo Edward Shayo.
Akisoma maelezo ya hati ya mashitaka
mbele ya mahakama hiyo ,Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu
mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa pili Edward Shayo (63) na wa
tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.
Kutokana na maelezo hayo Hakimu
,Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na
mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka
kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata
nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.
Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo
Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika
huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri
hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.
Hakimu Mkazi ,Mawore aliahairisha
shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu na
kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na kesi hiyo
kutokuwa na dhamana .
MWISHO.
No comments:
Post a Comment