Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza
jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya
Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo,
Jana Januari 4, 2018. Picha Zote Na
Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune mara baada ya kuwasili wilayani
humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana
na Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali mara baada ya
kuwasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja, Jana Januari 4, 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza
jambo wakati akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na kamati ya ulinzi ya
Wilaya ya Mbarali wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua shughuli za maendeleo,
Jana Januari 4, 2018
Na Mathias Canal, Mbeya
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe Mary Mwanjelwa amemuagiza
Mrajis Mkuu wa Maendeleo ya Ushirika nchini kuanza uchunguzi mara moja kwenye
SACCOS ya Wakulima wa mpunga Madibila iliyoko Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya ili
hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Watendaji waliohusika na upotevu wa
fedha pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Mhe Mwanjelwa alitoa agizo hilo Jana Disemba 4, 2018 wakati
akipokea taarifa ya kilimo ya Wilaya ya Mbarali akiwa katika ziara yake ya
kikazi Wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune alimueleza Mhe
Mwanjelwa kuwa katika SACCOS ya Madibila kumekuwa na hasara kubwa kutokana na
matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika.
Hivyo
alimuomba Naibu Waziri kuwachukulia hatua za kinidhamu haraka viongozi wote
waliosababisha hasara kwenye vyama hivyo vya ushirika baada ya uchunguzi
kufanyika katika kipindi cha siku 14.
Aliongeza kuwa taarifa ya ukaguzi iliwasilishwa kwa Mrajis wa
vyama vya ushirika kwa barua Kumb Na. MDC/C.20/10/89 tarehe 23/01/2017 lakini
mpaka sasa hazijachukuliwa hatua zozote za kinidhamu jambo ambalo linafifihisha
shughuli za wananchi kujipatia maendeleo endelevu.
Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa ametoa wiki mbili (siku 14) kwa
Mrajis kufika katika SACCOS hiyo ya Madibira na kutoa majibu haraka ya matokeo
ya uchunguzi huo katika kipindi tajwa.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa sekta ya ushirika ni moja kati ya
sekta muhimu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Vikundi, Wilaya, Mkoa na
Taifa kwa ujumla katika kukuza pato la mwananchi na kupunguza umasikini hivyo
ni lazima kuwa na majibu ya haraka pindi kunapobainika uhujumu wa vyama hivyo.
Alisema kuwa Viongozi wa Wilaya zote nchini wana jukumu muhimu
la kuhamasisha na kuhiza wanachama kuongeza thamani ya mitaji yao ili
kuviwezesha vyama kukuza mitaji ya ndani badala ya kuwa tegemezi kwenye Taasisi
zingine za kifedha.
Aidha, Kuendelea kutoa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ya Mazao
ghalani ili mkulima apate bei stahiki ya Mazao yake.
MWISHO
No comments:
Post a Comment