NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mkuranga
NAIBU
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.
Antony Mavunde, ameendelea kuwabana waajiri wanaokiuka sheria za nchi ambapo
leo Machi 8, 2018
amehamia wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani na kuvitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 32, viwanda vitatu kwa ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Kazi na Uhusiano Mahala pa Kazi.
amehamia wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani na kuvitoza faini ya jumla ya shilingi milioni 32, viwanda vitatu kwa ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Kazi na Uhusiano Mahala pa Kazi.
Viwanda
vilivyoadhibiwa ni pamoja na kiwanda cha kutengeenza yeboyebo cha Dorin
Investment Company Limited, (milioni 14), LM Furniture, (milioni 7), na
Tingtang, (milioni 14), adhabu hizo zimetangazwa leo Machi 8, 2018 na Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe.
Antony Mavunde wakati wa ziara yake ya kushtukiza ili kubaini waajiri ambao
wanakiuka sheria ya kazi na uhusiano kazini, na wale ambao bado hawajajisajili
na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri, viwanda hivyo vimekiuka sheria kwa kuhatarisha maisha na
afya za wafanyakazi kutokana na mzingira hatarishi ikiwa ni pamoja na
wafanyakazi kutokuwa na vifaa vya kujihami (protective gears), kufanya kazi
masaa mengi bila ya kulipwa malipo ya muda wa ziada ambao uko nje ya muda wa
kisheria wa mfanyakazi kufanya kazi.
Aidha
Naibu Waziri ameagiza uongozi wa viwanda hivyo kuwasilisha nyaraka muhimu kwa Kamishna wa Kazi, Jumatatu ijayo kwani
nyaraka nyingi walizotakiwa kuzionyesha hawakuwa nazo, ikiwa ni pamoja na
mikataba ya kazi, salary sleeps za wafanyakazi wao.
Sambamba
na hilo Mheshimiwa Mavunde ameuagiza Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF),
kumfikisha mahakamani mara moja mwajiri wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya
plastiki, cha Tisino kwa kutojisajili na WCF kama sheria inavyotaka.
Naibu
Waziri Mvunde yuko katika ziara ya kuwabaini waajiri ambao hawatekelezi
ipasavyo Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini, na wale ambao bado hawajajisajili
na Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), na kuonya kuwa waajiri wote ambao
bado hawajatekeleza takwa la kisheria la kujisajili WCF watapelekwa mahakamani
na serikali haitabadili msimamo huo hadi hapo matakwa ya kisheria
yatakapotekelezwa na waajiri wote nchini.
Naibu Waziri Mavunde akitoa maagizo kwa viongozi wa kiwanda cha kutengeenza viatu vya plastiki (yeboyebo), cha Dorin.
Naibu Waziri Mavunde, akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha LM Furniture ambaye licha ya kufanya kazi ya kuhamisha vitu vyenye ncha kali, kama vyuma na mabati hakuwa amevaa gloves, wala viatu vigumu (gumboots). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bi. Rehema Kabongo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Mhe. Filberto Hassan Sanga (katikati), akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano -WCF, Bi. Laura Kunenge.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Mhe. Filberto Hassan Sanga (katikati), akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, (wapili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bi. Rehema Kabongo, (wakwanza kushoto) na Meneja wa kiwanda cha Tingtang, Bw. Lee.
Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
Wafanyakazi kiwanda cha Tingtang
Mhe. Mavunde akimsikiliza Meneja wa kiwanda cha Tingtang, Bw. Lee.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Dorin, wakimsikilkzia Mhe. Mavunde, alipozungumza nao
Maafisa wa juu waliofuatana na Mhe. Mavudne wakiwa pamoja na maafisa wa Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Mkuranga.
Bw. Lee akijieleza mbele ya Mhe. Mavunde, na Kamishna wa Kazi, Bi. Hilda Kabisa,
No comments:
Post a Comment