Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018. Picha Zote Na MathiasCanal-Wazo Huru Blog
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini (Kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.
Mhe Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.
Maandamano ya wanawake wakielekea katika dhifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika Wilayani Bukombe, Leo 8 Machi Machi 2018.
Na Mathias Canal, Bukombe-Geita
Mwanamke si mtu wa kubezwa kama ilivyo desturi na mtazamo wa
wengi kwamba mwanamke hawezi kufanya jambo lolote kama hatawezeshwa, Hii ni
dhana mfu tena iliyopitwa na wakati tumejionea wanawake wangapi ambao
wanawawezesha wanaume tena bila hata wao kuwezeshwa.
Hayo yamesemwa Leo 7 Machi 2018 na Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Madini wakati wa
maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo katika Mkoa wa Geita yamefanyika
Wilayani Bukombe na kusisitiza kuwa watanazania hawapaswi Kuishi kwa kukariri
ni hatari kwa ustawi wa maisha yetu hivyo ni vyema kama tutaishi kwa kujifunza
maana hata tafsiri ya maisha nyepesi ni ile ya kuishi na kujifunza.
Alisema kuwa Katika Jamii mara kadhaa yameripotiwa matukio
mbalimbali ikiwemo yale ya kuwanyanyapaa wanawake, kuwapiga lakini yapo pia
matukio ovu kabisa ya kuwabaka wanawake jambo ambalo Serikali inaendelea na
juhudi za makusudi kukomesha madhila hayo.
"Mwanamke ana heshima kubwa ya Jinsia yake lakini pia
Wanawake ni mama zetu, dada zetu, wake zetu, wadogo zetu, shemeji zetu,
shangazi zetu lakini pia ni Nyanya (bibi) zetu" Alikaririwa Mhe Biteko na
kuongeza kuwa
Kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka 2018 isemayo “Kuelekea
uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na uwazeshaji wa wanawake
vijijini” inasisitiza kuwajengea wanawake uwezo wa kitaaluma, Kibiashara,
Upatikanaji wa mitaji, Masoko na Mikopo ili waweze kushiriki kwa usawa na
kunufaika na fursa zilizopo badala ya kuwa wasindikizaji tu.
Maadhimisho ya wanawake Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo
Machi 8, ambapo inaelezwa kuwa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Duniani kwa
mara ya kwanza yalifanyika Februari 28, 1909 huko Marekani.
Umoja wa Mataifa wenyewe umesema siku hii ni ya kutafakari juu
ya hatua za kimaendeleo ambazo wanawake wamepiga, kupongeza juhudiza wanawake
wa kawaida kutokana na mchango wao katika historia ya maendeleo ya nchi na
jamii zao.
Mbunge huyo wa Bukombe Mhe Biteko alisisitiza kuwa maadhimisho
hayo yaifanya kuwa siku ambayo wanawake hutambuliwa kwa mchango na mafanikio
yao bila kujali mipaka ya kitaifa, rangi, lugha, utamaduni, uchumu wala siasa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment