Tuesday, July 31, 2007

Miss tanzania alitema buzi!!


Miss Tanzania 2004, Faraja Kota anadaiwa kumtema mpenzi ‘buzi’ wake wa zamani, Masumbuko Kebacho baada ya fedha alizoiba kijana huyo (shilingi milioni 400) kumalizika, Risasi limeambiwa.

Habari za uhakika kutoka chanzo chetu, kilimpasha mwandishi wetu hivi karibuni kuwa Kabecho sasa anafanyakazi ya uhudumu wa baa kwenye Hoteli iitwayo Kilimanjaro iliyopo mjini Lilongwe, Malawi.


Kabecho ambaye aliiba shilingi milioni 400, kwa mfanyabiashara mmoja maarufu nchini mwanzoni mwa mwaka jana, alikimbia na kutumbua pesa hizo kwa starehe huku akishirikiana na Faraja Kota kabla ya kutorokea Afrika Kusini .


Kutokana hali hiyo Jeshi la Polisi wa Kimataifa (Interpol) walipewa taarifa juu ya wizi huo pamoja na kutoroka kwa kijana huyo ambapo walimsaka bila mafanikio.


Habari zinasema kuwa awali Kabecho alikuwa akiwasiliana na Faraja, huku akimtumia baadhi ya fedha lakini alipoishiwa kabisa mrembo huyo alikata mawasiliano naye.


Mtoa habari huyo alisema kuwa, ilifikia wakati ambapo Kabecho akipiga simu, mrembo huyo alikuwa haipokei au huikata mara alipogundua aliyekuwa akimpigia, kitendo kilichomsononesha sana kijana huyo.


“Baada ya kugundua kuwa fedha alizokuwa nazo zimeisha, Faraja alikuwa hapokea simu yake tena na kumfanya Kabecho wakati mwingine alie kwa hasira hasa akimbuka mapenzi yao alipokuwa na fedha,” alisema mtoa habari huyo.


Habari zaidi zinasema kuwa baada ya muda Kabecho alihama Afrika Kusini na kuhamia Malawi.

Akiwa nchini humo, hali yake kifedha ilikuwa mbaya hivyo, aliamua kutafuta kazi ya uhudumu wa baa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro iliyopo Area 9 ya mjini Lilongwe inayomilikiwa na dada mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Josephine.


“Hali ilikuwa mbaya sana kwa kijana huyo lakini sasa angalau kidogo anaweza kupata hela ya chakula baada ya kupata kibarua hicho kwenye baa,’’ alisema mtoa habari huyo ambaye alidai kuwa anamjua vizuri Kabecho.


Wakati Kabecho akiwa katika hali ya ukata, Faraja sasa anadaiwa kujitosa kwa mbunge mmoja kijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (jina tunalihifadhi).

Imedaiwa kuwa mrembo huyo hivi sasa hasikii wala haoni kwa mheshimiwa huyo ambaye anampatia huduma zote zinazostahili kwa wapendanao.

“Kwa ujumla, hivi sasa Faraja anatesa na mbunge huyo kijana ambaye anamtimizia kila atakacho,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Kigogo ‘aparalaizi’ akizini na hawara

Na Mwandishi Wetu



Kigogo mmoja wa kampuni tangu ya uingizaji na uuzaji wa mafuta nchini (jina tunalihifadhi) Jumanne ya wiki iliyopita alijikuta akikumbwa na maswahibu mazito baada ya ‘kuparalaizi’ akiwa anafanya tendo la ndoa.


Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, ambaye hakupenda jina lake kuandikwa gazetini, tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 11.00 katika nyumba ya kulala wageni ya Masco iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.


Habari zinadai kuwa, kigogo huyo alitinga katika gesti hiyo na kukodi chumba namba 9 akiwa na hawara yake aliyejulikana kwa jina moja la Kibibi.


Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo anayeishi eneo la Temeke alitinga na mpenzi wake kwa lengo la kupeana raha lakini katika hali ya kushangaza wakiwa katikati ya tendo, kigogo huyo alianza kulalamika ya kuwa anahisi upande wake wa wa kushoto unapoteza nguvu.


Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya kigogo huyo kulalamika hivyo, hawara yake alisitisha zoezi walilokuwa wakifanya kisha kuanza kuchunguza kilichokuwa kikimsibu mpenzi wake ndipo alipobaini jamaa alikuwa ‘ameparalaizi’ upande wote wa kushoto.


Kutokana na hali hiyo Kibibi alichukuwa simu ya kigogo huyo na kuanza kupekuwa majina yaliyokuwemo na kufanikiwa kuona jina lililoandikwa ‘wife’ ambapo alimpigia na kumfahamisha yaliyojiri na eneo walilokuwepo kisha alitoweka.


“Kibibi alitoka chumbani akiwa amechanganyikiwa, tulimuuliza kilichomkumba akadai kuwa kigogo aliyekuwanaye ‘ameparalaizi’ ghafla, hivyo amempigia mkewe kumfahamisha,” kilisema chanzo hicho.


Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kimada huyo alisema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kuona kigogo huyo anashindwa hata kuongea.


Habari zaidi zinasema kuwa mke wa kigogo huyo alikwenda Kituo cha Polisi cha Chang’ ombe na kutoa taarifa ambapo askari walikwenda eneo la tukio na kumkuta akiwa hoi.

Chanzo hicho kilisema kuwa askari hao kwa kushirikiana na watumishi wa gesti hiyo, walimchukuwa kigogo huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa matibabu.

Kwa mujibu wa habari hizo, kigogo huyo alilazwa na kupatiwa matibabu hadi Alhamis ya wiki iliyopita ambapo alihamishiwa katika Hopitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke, Emmanuel Kandihabi akiongea na mwandishi wetu alisema kuwa taarifa hiyo haijapata lakini aliahidi kuifanyia kazi.


1 comment:

Anonymous said...

huyu dada nae anapenda mijitu iliyoshiba. si alimtema Aggrey mareale pia.