Wednesday, July 4, 2007

SARANDA HIYOOO!!!!


Train inapofika stesheni maarufu ya saranda, watu kibao hushuka na kutafuta chakula. mlo maarufu unaopatikana hapa ni nyama choma ya kuku, lakini kitu kimoja wengi wanakipuuzia ni mazingira ya kuandaa kuku hao. mara nyingi nyama yake huwa mbichi na wakati mwingine unapokula unaweza kuona damu!! Kwa wale wanaojali afya zao, hapa siyo mahali pazuri pa kula nyama, acheni uchu mtapoteza maisha kwa kupenda vya dezo. After all nani ana uhakika hao ni kuku na siyo wale ndege waitwao 'kimeza nyoka?"

1 comment:

Anonymous said...

Kimsingi ni bombe la ushauri, bila shaka kwa wale wanaopita njia hii, watajifunza. Maana unaweza kula hata bundi bila kujua!
Umeniacha hoi kusema kuwa nyama nyingine unaweza kula zikatoa damu...kweli hapo kazi ipo!!! Kwani hakuna chakula kingine zaidi ya hao kuku ambao ni hatari?