Christopher Lissa na
Richard Bukos
Tamasha kubwa la burudani la Fiesta mwaka 2007, lililofanyika Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, liliharibiwa na mvua pamoja na kutawaliwa na vioja vya kila aina.
Timu ya waandishi wa Ijumaa Wikienda ambayo ilikuwepo Leaders ili kuripoti ‘live’ Fiesta 2007, waliweza kushuhudia vitendo vya ngono vikitawala pembezoni mwa viwanja hivyo huku jukwaa la wasanii likigubikwa na vurugu za kila mara.
Wasanii wakubwa walioalikwa kutoka nje ya nchi, Mjamaika Kelvin Lyttle na Mkongomani Koffi Olomide, walishindwa kukonga nyoyo za mashabiki na kujikuta wakifunikwa na bendi za hapa nyumbani kama Akudo Impact na FM Academia.
Kwa kutambua ukubwa wa shughuli hiyo na matukio mengi mchanganyiko yaliyokuwa yakijiri kwenye Viwanja vya Leaders siku hiyo, timu ya wandishi wetu ilikuwa ikiwasiliana ‘live’ na makao makuu ya gazeti hili, yaliyopo Kariakoo, jijini Dar es Salaam.
Mawasiliano yalikuwa kama ifuatavyo;
Saa 5 asubuhi
Leaders: Mkuu milango ndiyo imefunguliwa, watu ni wachache, lakini kusema ule ukweli leo kazi ipo, ulinzi ni mkali kuliko, mbwa wametanda, polisi, Black Ninjaz na mabaunsa, yaani mpaka kuingia uwanjani lazima upitie hatua tatu na ukaguliwe kwa vifaa maalumu.
Makao Makuu: Vipi hali ya hewa ya leo, unadhani tamasha litafana kama kawaida yake?
Leaders: Inawezekana si unajua Wabongo kwa kupenda mambo haya ya kujirusha, lakini kuna hali fulani ya manyunyu na wingu limetanda, hii inaweza kuharibu shughuli au baadaye mambo yanaweza kuwa safi:
Dakika 15 baadaye
Leaders: Tumeshangia ndani kuna utofauti mkubwa ambao tunauona leo, tunaona jukwaa kubwa ambalo sidhani kama nitakosea endapo nitasema lina hadhi ya kimataifa, tunaona pia mahema kila sehemu ambayo yameandaliwa kwa ajili ya huduma mbalimbali kama chakula, vinywaji na matibabu.
Pamoja na hivyo, mimi naona tuwasiliane Saa tisa muda ambao ndiyo ‘shoo’ itaanza, hii ni kwa mujibu wa ratiba.
Saa 9 alaasiri
Leaders: Jamani hapa sasa tunaanza kushuhudia utani, tuliambiwa saa tisa ndiyo ‘shoo’ inaanza, lakini sasa hivi ndiyo kwanza watu wanaanza kurekebisha vyombo vya muziki, na saa yangu inanionesha sasa hivi ni saa tisa na nusu.
Makao Makuu: Ok, basi endeleni kufanya tathmini, lakini ‘shoo’ itakapoanza msiache kuwasiliana na sisi.
Saa 2 kamili usiku
Leaders: Naam shughuli sasa ndiyo inaanza, si unajua tena uswahili, saa tisa imekuwa saa mbili.
Wanaanza kupanda wasanii chipukizi kwa zamu.
Makao Makuu: Basi, msishangae muziki peke yake, jigaweni kuzunguka kila pembe za uwanja ili mtwambie kila kinachoendelea.
Saa 6 usiku
Leaders: Mvua inaharibu pozi hapa, FM Academia ndiyo wapo jukwaani, lakini manyunyu yanawakimbiza watu, wengi wamekwenda kujificha kwenye mahema lakini wengine wamejifunika viti, hata hivyo Wazee wa Ngwasuma siyo mchezo wanatawala jukwaa siyo kawaida, wanashangiliwa kwa sana tu.
Makao Makuu: Kabla ya Academia, ni makundi gani yalipanda jukwaani?
Leaders: Kuna Chipolopolo, Sikinde, Msondo, DNA wa Kenya, Ngoni wa Uganda na wasanii wengine chipukizi.
Saa 8 usiku
Leaders: Mnamjua Koffi?
Makao Makuu: Yap, Chales Antoine Olomide, amefanya nini?
Leaders: Ndiyo amemaliza kazi yake jukwaani, lakini ilikuwa ni ‘mdebwedo’, hakukonga nyoyo za mashabiki kama ilivyotabiriwa, ingawa alishangiliwa kiasi fulani, kusema ule ukweli amefunikwa na FM Academia na Akudo Impact.
Kingine ni matukio ya pembeni, kuna washkaji ambao hawana habari na burudani, wao wamejitenga wanawake kwa wanaume na kupeana mahaba mazito gizani, wengine wametandika kanga, wamelala, yaani ni vitendo vya ngono tu ndiyo vinavyojiri kwenye kona za uwanja.
Saa 10 usiku
Leaders: Wanamuziki wa nje ni hoi tu, yaani huwezi kuamini muda mchache uliopita Kelvin Lyttle ndiyo amemaliza kuimba lakini hakuleta shangwe wala nini, alijaribu kidogo alipoimba wimbo wake maarufu wa Turn me on na mashabiki wakawa wanamuitikia vizuri.
Saa 12 asubuhi
Leaders: Kumeshapambazuka na fiesta ndiyo inaelekea ukingoni, lakini kuna matukio mengi yaliyotokea hapa katikati, tunataka tueleze moja baada ya lingine.
Makao Makuu: Endeleeni.
Leaders: Jay Moe alipatwa na bonge la ‘soo’, alipopanda jukwaani kuimba mashabiki walianza kumzomea, lakini mbaya zaidi walikosa simile na kumrushia makopo yenye mikojo, lakini mabaunsa walimkamata shabiki mmoja na kumshushia kipigo cha nguvu.
Jambo lingine ni Kamanda wa Kikosi cha Mizinga, Kalapina alikunjiana ngumi na Ma-Dj ambao walimzimia muziki, pia Fid Q muda mwingi alikuwa chemba akikumbatiana na kimwana mmoja hivi, sijui ndiye demu wake mpya?
Kitu cha kufurahisha kilichotokea kwenye fiesta hii ni Juma Nature kutinga jukwaani na kukamua pamoja na kundi lake la Wanaume Halisi, si unajua Nature ni baba harusi, basi ametoka kwenye reception (sherehe baada ya ndoa) na kuja moja kwa moja kuimba.
Hata hivyo, alifanya kazi nzuri, alifunika na mashabiki walimshangilia si kawaida.
ZITTO KUTINGA IKULU
Na Elvan Stambuli
Kuna kila dalili kwamba Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe atatinga Ikulu ili kumueleza Rais Jakaya Kikwete kile ambacho anaamini kiongozi huyo wa nchi alipitwa kisogoni na mkataba wa madini ukatiwa kinyume na amri yake aliyoitoa Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam juzi, Zitto atalazimika kwenda Ikulu ama kwa kuitwa na ofisi hiyo au chama chake kutaka kufanya hivyo ili Rais Kikwete apewe taarifa kwa undani zitakazomsaidia kuchukua hatua zinazofaa.
Mgombea Ubunge wa CHADEMA Jimbo la Kinondoni mwaka 2005, Hassein Yahya alisema alipozungumza na gazeti hili katika viwanja hivyo kuwa ili Rais Kikwete asipotoshwe, angeshauri mkuu huyo wa nchi kukutana na Zitto moja kwa moja.
Alisema hakuna njia ya mkato katika kupatia ufumbuzi jambo analolalamikia Zitto isipokuwa ni kuonana ana kwa ana na Rais Kikwete.
“Akionana na Rais Kikwete atamfahamisha kuwa amri yako uliyoitoa ya kupiga marufuku kusainiwa mikataba mipya imepuuzwa, nasema hivyo kwa sababu aliutangazia umma hivyo na hatujasikia tangazo la kuruhusu watendaji wa serikali kuingia mikataba mipya na nchi za nje, “ alisema Hassani.
Mwananchi mwingine , Bi Saida Mwagagana alisema ni vema Rais Kikwete akaketi na Zitto ili kuona kile ambacho alitaka kifanyiwe uchunguzi na akigundua kuwa kuna ukweli ndani yake basi achukue hatua zinazostahili.
Aidha wananchi wengi waliohojiwa katika viwanja hivyo walishauri viongozi wa CHADEMA kufanya kila wawezalo ili kuonana na Rais Kikwete ili ikiwezekana Zitto aondolewe adhabu kwani alichokuwa akidai ni kwa maslahi ya taifa.
Naye Wakili maarufu nchini Bw. Mabere Marando akizungumza na gazeti hili katika viwanja hivyo alisema Spika wa Bunge Bw. Samueli Sita amesahau sheria kwa kumfungia Zitto kuhudhuria vikao vya bunge mpaka mwakani kwa kuwa kanuni za bunge hazisemi hivyo.
Marando ambaye amewahi kubwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la Afrika Mashariki alisema kanuni za bunge zinataja kuwa mbunge akikosa mara ya kwanza anafungiwa siku tano, kosa la pili siku 20 na kosa la tatu bunge hujadili iwe ziku ngapi.
“Spika Sitta ni wakili wa zamani, amesahahu sheria, sasa ni wazi kwamba amefanya kosa katika hili, hakupasa kumfungia siku zote hizo hata kama Zitto ana kosa, “ alisema Marando.
Akihutubia umati mkubwa wa watu katika Viwanja vya Jangwani juzi Zitto alidai kuwa Waziri wa Madini, Nizar Karamagi alisaini mkataba wa madini nchini Uingereza huku Rais Kikwete akiwa hana habari,
Hadi tunakwenda mitamboni Ikulu ilikuwa haijatoa tamko lolote kuhusiana na sakata hilo la mkataba wa madini na Zitto.
Zitto alisimamishwa bungeni wiki iliyopita na atatumikia adhabu ya kutojihusisha na shughuli zozote za bunge hadi Januari mwakani, hiyo ilitokana na wabunge wengi kuona mbunge huyo alisema uongo na kumchafu Waziri Karamagi.

No comments:
Post a Comment