TUKO MSTARI WA MBELE KUSAIDIA JAMII, HATUNA TAMAA YA PESA!
Hivi ndivyo alivyokuwa akiishi binti huyu, alisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu, lakini baada ya kuonwa na Uwazi, tuliandika habari zake na kuhimiza Watanzania kumsaidia na hatimaye kufanikiwa kupelekwa India alikofanyiwa oparesheni iliyobadili maisha yake kupitia Global Publishers!Baada ya matatizo ya miAka kadhaa aliyoyapata kabla ya kuonwa na Global Publishers, hatimae binti huyu maarufu sasa, Ngendelaki Idd, anaishi maisha ya furaha akiwa ameolewa na ana watoto, katika watu ambao kamwe hawataisahau Global Publishers katika maisha yao, ni pamoja na huyu. WE CHANGE PEOPLE'S LIVES! Kabla ya kuonwa na kamera za Global Publishers, hali yake ilikuwa hivi binadamu huyu! Baada ya kufanyiwa operesheni na kurudi katika hali yake ya kawaida kwa gharama za Global Publishers.Kabla ya kufanyiwa oparesheni, suruali kwake ilikuwa ni 'luxury' Baada ya kufanyiwa opareshini na kuweza kuvaa 'mkanda nje' tena Alivyokuwa kabla ya kufanyiwa oparesheni Alivyo sasa baada ya kufanyiwa opareshini katika hospitali ya Dr. Mvungi Kinondoni jijini Dar kwa gharama za Global Publishers, kupitia kitengo chake cha Community Project.
1 comment:
Hahaa Kusaidiana ni swala la kila mtanzania hiyo Global Publisher kama imesaidia watu 20 au hata 30 katika matibabu ni vizur na niwa jibu na sio wewe peke yako unaesaidia hata hilo gazeti la KULIKO ambalo ametoka MHESHIMIWA CHAHALI Ambae Mkurugenzi wake ni MHESHIMIWA MENGI wao wamefanya mengi mengi mengi mengi mengi tena mengi saaaana nadhani hayataesabika nadhani mnamjua mengi alivyokuwa MTU mbele ya watu na anaethamini UTU kuliko KITU, NA NDO MAANA VYOMBO vyake vya habari havipendi shusha hadhi maisha ya mtu hata siku moja.
Nyinyi Global mshabadilisha maisha ya watanzania kwa style nyingi! mmewasaidia wengine wamepona maradhi na wanaishi kwa raha na amani sawa hilo hata watu wa kawaida wanafanya kulingana uwezo wao sio swala la kujisifia NA SIKU ZOOOTE MWENYE ROHO MBAYA AKISAIDIA LAZIMA ASEME SABABU SIO KAWAIDA YAKE KUSAIDIA.
Hapo hapo Global Publishers Mnabadilisha maisha ya watu kwa kuwaponzea aidha ndoa zao kuwa kwenye vurugu au watu kuachana kabisa,au kumshusha mtu hadhi kwenye fani yake kwa habari zenu hizo ambazo vyanzo vyake vingi ni uongo (wanawadanganya, juzi hapa nimesoma habari ya changudoa sijui wa wapi huko hakukuwa na sababu ya kutaja na jina la mzazi wake na anakoishi hata kama yule binti ametaja, ulipaswa kutaja jina la yule binti na ubini wake inatosha na sio kutupa maelezo ya baba yake mpaka anapoishi ile NI KUMDHALILISHA YULE MZEE, baba yake sie aliemtuma kwenda kufanya yale mambo!!! hapo pia mmebadilisha maisha ya mtu???
CHAHALI IS A WINNER!!!! CONGRATS.
Post a Comment