Monday, March 15, 2010

PENDO AAGWA!

Buriani Pendo!
ndugu na jamaa wa marehemu wakilia kwa uchungu
mama wa marehemu Pendo (katikati)
Binti Juliet Mrina 'Pendo', ambae alikuwa girlfriend wa mwanamuziki wa bongo flava Madee, aliyeaga dunia wiki ilkiyopita katika ajali ya basi la Shabiby akielekea Dodoma, leo ameagwa katika Hospitali ya Muhimbili kabla ya maziko yatayoyafanyika nyumbani kwao Rombo, Moshi kesho. Eneo la kanisa la Muhimbili lilijawa na majonzi wakati wasanii mbalimbali, ndugu na marafiki wa Madee na Pendo walipojitokeza kuuaga mwili wake. Ilikuwa inatia simanzi kwa sababu ajali imekaztiza ndoto nyingi alizokuwa nazo Pendo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John kilichopo Dododma na alikuwa katika mwaka wake wa mwisho uliotarajiwa kufikia tamata mwezi Juni mwaka huu!!
Mungu ailaze Roho yake peponi - Amin

No comments: