Tuesday, September 25, 2007

Binti atolewa vitu tumboni


Vitu vinavyoonekana juu ya trei pembeni ya binti huyo ndivyo vilivyotolewa tumboni mwake...tuna madaktari kweli au...?
Binti mmoja ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mkuranga iliyopo Mkoani Pwani, Bi. Leah Saisai Aminiel amenusurika kufa baada ya Daktari aliyekuwa akimfanyia operesheni ya kujifungua kudaiwa kusahau vipande vya bandeji tumboni.

Akiongea na mwandishi wetu katika Hospitali ya Mikocheni iliyopo jijini Dar es Salaam alikolazwa akitibiwa, Mwalimu huyo alikuwa na haya ya kueleza;

''Sijui hatma ya maisha itakuwa nini ili ligundulike tatizo linalo nisumbua natakiwa nifanyiwe kipimo kikubwa kwa gharama ya shilingi 350,000 katika Hospitali ya Agakhan.

Matatizo niliyonayo yalianza baada ya kufanyiwa operesheni ya kujifungua Januari 12, mwaka huu katika Hospitali ya Serikali Temeke.

Baada ya kupita wiki moja tangu nifanyiwe operesheni hiyo niliondolewa nyuzi na kuruhusiwa kurudi nyumbani nikiwa na mwanangu Shadrack lakini jambo la ajabu tumbo langu liliendelea kuwa kubwa kama vile nilikuwa sijajifungua.

Nilikwenda hospitali ya Muhimbili ambako nilifanyiwa vipimo na kukutwa sina tatizo. Nikaanzishiwa dozi ya kifua kikuu

Julai 7 niliamua kwenda kujaribu tiba katika Hospitali ya Mikocheni ya Kagaruki, nilipogunduliwa kuwa na kulikuwa na pamba tumboni.

Kutokana na hali hiyo daktari huyo alinifanyia operesheni na kunitoa pamba tano lakini alishindwa kumalizia kunishona baada ya kuishiwa damu. Hata hivyo hali yangu sasa inaendelea vizuri,” alisema mwalmu huyo ambaye anaomba msaada kwa watu wenye huruma ili aendelee kupata tiba kwa madai kuwa gharama ni kubwa.

Kama utapenda kumsaidia Mwalimu huyo unaweza kuwasiliana naye kwa namba +255 0754-039092, 0754-362990.

No comments: