Tuesday, September 25, 2007

SOPHIA BADO ASUBIRI HATMA YAKE!


Mwandishi mwandamizi wa magazeti ya Global Publishers, Dotto Mwaibale, akikabidhi, kwa niaba ya kampuni ya Global Publishers, shilingi 200,000 kwa Sophia, ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba miguu. Hivi sasa binti huyo yu ngalipo hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam akisubiri hatma yake kufuatia ahadi na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Watanzania waishio Ulaya na Marekani walioahidi kumsaidia baada ya kuona taarifa zake kupitia Blog hii.
Kufuatia maombi mengi ya Watanzania waishio nje ya Tanzania, baba mzazi wa Sophia amefanikiwa kufungua akaunti katika benki ya Standard Chartered. Kwa wale watakaotaka kutoa misaada yao ya kifedha, jina la akaunti ni Mwiga Francis Aloyce; Accnt No. 0150101067800.

..akiwa na baba yake mzazi....

No comments: