Saturday, September 15, 2007

Waraka wa Shigongo kwa wasomaji wa gazeti la Ijumaa


Ndugu wasomaji,

Naomba nichukue nafasi hii, kwa niaba ya kampuni, nikiwa Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa magazeti pendwa ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi, Risasi, Amani na The Bongo Sun. Pia kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hii, nachukua fursa kuwaomba radhi ninyi wasomaji kwa kilichotokea katika habari na picha zilizochapishwa kwenye gazeti la Ijumaa la tarehe 14, Septemba, 2007, chini ya kichwa cha habari WABAMBWA!

Asubuhi na mapema siku ya Ijumaa baada ya gazeti hilo kutoka, nilianza kupokea simu kutoka kwa wasomaji wengi wanaotutakia mema wakidai habari hiyo ilikuwa ni ya kweli lakini haikutokea nchini Tanzania kama tulivyoandika, bali nchi jirani na kwamba ziko kwenye mtandao. Simu hizo zilinishtua sana, nikalazimika kulitafuta gazeti hilo ili nisome na kuona kama taarifa nilizopewa zina ukweli wowote.

Baada ya kuziona picha hizo na kuisoma habari husika, nilichofanya ni kumuita mhariri wa gazeti hilo na kutaka atoe maelezo juu ya malalamiko yaliyotolewa na wasomaji wetu. Katika maelezo yake, mhariri alidai habari hiyo ililetwa na chanzo cha habari ambacho siku zote tumekuwa tukifanyanacho kazi na kukiamini. Kwa mujibu wa chanzo hicho, tukio hilo lilitokea maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam na kikafanikiwa kupiga picha hizo na kuzileta ofisini kwetu na kudai malipo ya shilingi 200,000 (laki mbili) zilizotakiwa kulipwa siku ya Ijumaa baada ya gazeti kutoka.

Kufuatia utata huo, niliagiza chanzo hicho kuhojiwa kwa mara nyingine kama kweli picha hizo zilipigwa Mabibo na yeye ama la, jambo hilo lilifanyika
na awali katika maelezo yake, chanzo kilisisitiza kuwa picha hizo alizipiga yeye katika eneo hilo, lakini baadaye alipobanwa kwa maswali mengi ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa picha kama hizo zilizotumwa kwetu kwa njia ya mtandao na msomaji aitwaye Anna, alikiri kudanganya kwa lengo la kujipatia fedha!

Kwa kweli, jambo hili, mimi binafsi pamoja na wenzangu katika Global, limetuumiza sana, kwani kwa muda mrefu yamekuwepo madai kwamba habari tunazoandika siyo za kweli, lakini mara nyingi tumefanikiwa kuwathibishia wasomaji wetu kuwa hatuandiki uongo. Ndani ya miaka kumi tunayokaribia kuimaliza, hata siku moja hatujawahi kupata tatizo la aina hii! Hii ni mara ya kwanza, tunakiri kosa hili na tumeshaelewa tatizo letu, tunaahidi kuwa makini zaidi siku nyingine ili tusiudanganye tena umma wa wasomaji wetu wanaotuheshimu na kununua magazeti yetu kila siku.

Zipo hisia kwamba, chanzo hiki kilikuwa kimetumwa na maadui zetu kwa lengo la kutushushia heshima. Jambo hili bado tunalifanyia kazi, lakini tunachokifahamu ni kwamba mwisho wa vita vilivyopo tutashinda tu kama ninyi mtaendelea kusimama na sisi na kutukosoa pale tunapokwenda vibaya. Kumbukeni “to grow economically you need friends, but to develop economically you need enemies, so enemies are important for us to develop.”

Hatua makini zimechukuliwa kwa chanzo hiki, kisingeweza kuachwa kiondoke huru baada ya kuwa kimetuumiza kiasi hiki. Kinachoendelea wakati tunaandika waraka huu, ni kwamba Bw. Anos Magongo yuko Kituo cha Polisi Msimbazi, alikamatwa siku hiyo hiyo ya Ijumaa na kufikishwa kituoni ambako alifunguliwa kesi namba MS/RB/10757/07 ya kujaribu kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu. Anategemea kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Hizi ndizo hatua tulizozichukua, pamoja na yote hayo, hakuna jambo lolote ambalo muungwana anaweza kusema baada ya kukosea zaidi ya kuomba msamaha! Kwa niaba ya wenzangu, tunaomba mtusamehe na tunaahidi kuwa makini sana siku nyingine. Ni matumaini yetu mtakubali kufanya hivyo. Kumbukeni hili ni kosa letu la kwanza na sisi ni ndugu zenu, tumetoka nanyi mbali miaka kumi iliyopita, TUPENI NAFASI NYINGINE.

Mungu awabariki sana.

Ahsanteni

Eric Shigongo James

NB: Hatua kali pia zimechukuliwa dhidi ya Mhariri wa gazeti la Ijumaa.
(Picha za Anos HAPA)

MICHUZI AIBUKA UPYA!

DEAR FRIENDS
I AM PROUD AND PLEASED TO INTRODUCE YOU TO www.tztimes.com THE PORTAL FOR MODERN TIMES TANZANIA WHOSE MOTTO IS TO BE ONE STEP AHEAD IN AS FAR AS NEWS ABOUT TANZANIA, THE DIASPORA AND ANY OTHER THAT IS RELEVANT TO TANZANIA AND HER PEOPLE IS CONCERNED.
BASED ON A THREE YEAR RESEARCH IT HAS COME TO OUR REALISATION THAT SO FAR VERY FEW OUTLETS ATTEMPT NOT ONLY TO GATHER NEWS AND IMAGES OF HAPPENINGS BUT ALSO MOST ARE LATE IN DISSEMINATING IT TO CONSUMERS. OUR RESOLVE IS TO FILL THAT VACCUM.
OF COURSE, THIS IS NOT AN OVERNIGHT UNDERTAKING THAT WOULD BE PERFECTED IN NO TIME, RATHER IT IS THE FIRST STEP TOWARDS A LONG SAFARI WHOSE DESTINATION IS WHERE ALL NEWS CONSUMERS WORLDWIDE ARE. THEREFORE, AT THE OUTSET ALLOW ME TO SAY THAT WHATEVER GLITCH ENCOUNTERED IS NOT INTENTIONAL NOR A NORM BUT AN ATTEMPT TO ATTAIN PERFECTION. WE THEREFORE WELCOME VIEWS, CRITICISIM AS WELL AS NEWER IDEAS THAT WOULD HELP US THRIVE.
YOU ARE ALSO WELCOME TO CONTRIBUTE NEWS, IMAGES AND VIEWS IN ANY OF THE SUBJECTS AVAILABLE IN www.tztimes.com INITIALLY IN VOLUNTARY BASIS AND WHEN THE TIME IS RIPE WE CAN NEGOITIATE TERMS DEPENDING ON RELIABILITY AND CREDIBILITY OF MATERIAL SENT.
YOU WILL NOTE THERE IS A VIDEO COMPONENT WHICH WE ARE POISED TO FILL WITH STUFF THAT ARE RELEVANT. THAT AND OTHER PARTS ARE STILL WORKED ON AND AFTER THIS TRIAL PERIOD IS OVER, AND WHICH WE PLAN TO MAKE IT AS SHORT AS POSSIBLE, SAY TWO WEEKS, WE SHALL HAVE WHAT YOU HAVE BEEN CRAVING FOR IN TERMS OF LOCAL VIDEO CLIPS.
WITH A VIEW TO CATER FOR A WIDER AUDIENCE THE LANGUAGE USED IS BOTH KISWAHILI AND ENGLISH.
NEED I SAY MORE?
THANK YOU,
SINCERELY
MUHIDIN ISSA MICHUZI
MANAGING DIRECTOR
EMEDIA (T) LIMITED

Friday, September 14, 2007

Thursday, September 13, 2007

KILIO CHA KUOGOPA SEGEREA!

shehena ya bangi, katika mahakama ya Kisutu
BW. Ibrahim Assioundru (35), Rai wa visiwa vya Komoro alishindwa kujizuia kulia baada ya kuambiwa utakwenda Segerea baada ya kukutwa na shehena ya Bangi! Zaidi bonyeza HAPA

Wednesday, September 12, 2007

Cancer Update from John Hopkins

This information is being circulated at Walter Reed Army Medical Center as well.Please circulate to all you know

No plastic containers in micro
No water bottles in freezer.
No plastic wrap in microwave...

A dioxin chemical causes cancer, especially breast cancer.

Dioxins are highly poisonous to the cells of our bodies. Don't freeze your plastic bottles with water in them as this releases dioxins from the plastic.

Recently, Edward Fujimoto, Wellness Program Manager at Castle Hospital, was on a TV program to explain this health hazard. He talked about dioxins and how bad they are for us.

He said that we should not be heating our food in the microwave using plastic containers...

This especially applies to foods that contain fat.

He said that the combination of fat, high heat, and plastics releases
dioxin into the food and ultimately into the cells of the body...

Instead, he recommends using glass, such as Corning Ware, Pyrex or ceramic containers for heating food... You get the same results, only without the dioxin. So such things as TV dinners, instant ramen and soups, etc., should be removed from the container and heated in something else.Paper isn't bad but you don't know what is in the paper. It's just safer to use tempered glass, Corning Ware, etc.
He reminded us that a while ago some of the fast food restaurants moved away from the foam containers to paper. The dioxin problem is one of the reasons...
-
Also, he pointed out that plastic wrap, such as Saran, is just as dangerous when placed over foods to be cooked in the microwave. As the food is nuked, the high heat causes poisonous toxins to actually melt out of the plastic wrap and drip into the food.
Cover food with a paper towel instead.This is an article that should be sent to anyone important in your life!

SEXY DENTI!

Denti huyu ana Makuu..muone na msome HAPA

Mnamuonea donge Maimatha!


Mbona yuko fresh tu mamaa Mai wa Jesse?!!

Tuesday, September 11, 2007

The Bongo Sun Mtaanii!!

Roller Skaters..Bongo Sun!

Vendor..Bongo sun.. lisome hapa: www.globalpublisherstz.com

YOU ARE WHAT YOU EAT


Madhara na jinsi ya kukabiliana na ukosefu wa choo!

Pengine naweza kusema kwamba matatizo mengi ya kiafya anayoyapata binadamu huanzia tumboni, hasa pale vitu vinapokuwa haviendi sawa humo. Chakula tunachokula kila siku, kinatakiwa kuingia tumboni na kusagwa, kuchujwa na masalia kutolewa nje kwa njia ya kinyesi.

Mchakato huo unaposhindwa kufanyakazi ipasavyo, masalia yanayobaki tumboni hugeuka na kuwa chanzo cha maradhi. Kwa kawaida mtu hutakiwa kupata choo sawa na anavyokula. Kama unakula mara tatu kwa siku, basi na choo hivyo hivyo, chini ya hapo ni mara mbili.

Kwa ujumla suala la ukosefu wa choo liko mikononi mwa mtu husika, kutokana na jinsi anavyokula na staili yake ya maisha anayoishi. Baadhi ya vitu vinavyosababisha mtu kupatwa na ukosefu wa choo ni kupenda kula chakula haraka bila kutafuna ipasavyo, ulaji wa kupindukia, unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji sigara.

Sababu nyingine ni kuwa na vidonda vya tumbo, msongo wa mawazo, kuwa na ugonjwa kwenye mfumo wa usagaji chakula na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku kama inavyopendekezwa, lita moja mpaka mbili kwa siku.

TIBA MBADALA YA UKOSEFU WA CHOO

Ili kuepuka tatizo la kutokupata choo, kabla ya kula mlo wako kunywa glasi moja ya juisi ya limao ili kuondoa gesi tumboni na kuweka mazingira mazuri ya kusagwa kwa chakula utakachokila. kama tatizo la kutokupata choo limekuwa ni la muda mrefu, kunywa juisi ya ukwaju pamoja na papai bivu (angalau nusu) asubuhi kabla hujala kitu chochote.

Juisi ya ukwaju (glasi moja au mbili) na tunda la papai, vimeoanekana kuwa njia ya uhakika ya kulainisha choo, njia hii inaweza kutumika kama tiba mbadala kwa wale wenye tatizo hili kwa muda mrefu.

Kwa kawaida juisi na papai hutoa matokeo mara moja na iwapo hutapata choo kikubwa kwa siku ya kwanza, basi endelea kwa siku mbili au tatu zaidi na utaona mabadiliko makubwa tumboni mwako.

Tiba nyingine mbadala ni kunywa maji ya kutosha kwa siku na unaweza kuyanywa kila baada ya saa 2 au 3 huku ukichangaya kidogo na matone ya limau. Kwa wale wenye tatizo kubwa zaidi, wanaweza kujichua tumboni kwa mafuta ya kitunguu swaumu au mafuta ya soya.

LISHE YA MWENYE MATATIZO YA UKOSEFU WA CHOO

Ili kujiepuesha kabisa na tatizo la kukosa choo, epuka kupenda kula na kushiba mpaka unashindwa kupumua vizuri, kula chakula kiasi kama ilivyo kawaida mara tatu kwa siku. Ongeza kiwango cha kunywa maji kwa siku na usipendelee kunywa chai au kahawa, badala yake kunywa tangawizi, abdalasini (herbal tea), n.k.

Aidha katika mlo wako wa kila siku, jiepushe kula vyakula vyenye mafuta au vilivyopikwa kwa kukaanga. Epuka matumizi ya sigara na pombe za kupindukia. Zingatia kanuni ya ulaji matunda, milo mitatu kwa siku na ukishindwa basi angalau kula tunda moja, laweza kuwa papai, ndizi, embe, tufaha, chungwa, n.k. Utakavyokula matunda kwa wingi ndivyo utakavyojiepusha na matatizo ya tumbo na matatizo mengine mengi ya kiafya.

USHAURI MWINGINE

Epuka kuvaa nguo zinazobana. Tembea kwa miguu, angalau kwa dakika 30 kwa siku kama njia mojawapo ya kufanya mazoezi. Punguza msongo wa mawazo kwa kupumzika na kujiliwaza. Usifanye mchezo wowote mgumu mara baada ya kula. Fanya mazoezi ya mara kwa mara, kwani ni mazuri kwa mfumo mzima wa usagaji chakula.

Kama una tatizo la kumaliza siku moja au zaidi bila kupata choo, jua una matatizo, usikae kimya, chukua hatua sasa ili kujiepusha na matatizo makubwa ya kiafya siku zijazo!

Tuonane tena kwa makala nyingine wiki ijayo.

NEW BABY BOY!

The Bongo Sun: New baby Boy in the house.......come on inside HERE
Rashida Wanjara.....maiden Bongo Sun girl on page15

Vimwana wa ngwasuma!

FM Academia kimwana kazini...!
Mamaa Maimatha wa Jesse... uso huo..!

Monday, September 10, 2007

SFARI YA MWISHO YA SHENAZ!

Hii nd'o safari ya mwisho ya Shenaz (PICHA NDOGO)ilivyokuwa Jumapili jioni katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es salaam...ni vigumu kuamini lakini mapenzi ya Mungu yametimia..Mungu ailaze roho yake peponi ..Amen!
(kama unaiona kwa mara ya kwanza gonga HAPA)

AJALI YA MBARALI YAUA SHENAZ!

Baadhi ya maiti zilizokutwa eneo la ajali ya Mbarali
Mdogo wa marehemu Shenaz mara baada ya kupokea habari za msiba wa dada yake

Mtambaji maarufu wa taarabu nchiniTanzania, Shenaz Salum (pichani juu), ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya mbarali..ni masikitiko, pata habari kamili: www.globalpublisherstz.com

WEMA AWEKWA KATI!

Penzi la Miss Tanzania mstaafu, Wema Sepetu, limezua bifu zito.. Ipate full sory HAPA: www.globalpublisherstz.com

Sunday, September 9, 2007

STREET VERSION : Mungu hakupenda tushinde!

Safu hii (Street Version) ilikuwa miongoni mwa mashabiki wengi wa soka waliofurika ndani ya Uwanja mpya wa Taifa ili kuipa faraja Stars ambayo ilikuwa na kibarua kigumu mbele ya Mambas wa Msumjibi, kwa bahati mbaya Watanzania tulikandamizwa na Wamakonde hao bao moja bila majibu.

Baada ya mechi ‘Street Version’ ilisogea karibu na benchi la Stars ili kusikia maoni ya kocha na vijana wetu hao ambao baadhi yao walionekana kutokwa na machozi, pale walipokuwa wakihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari. Neno kubwa kutoka midomo mwao lilikuwa ni ‘Mungu hakupenda tushinde’.

Jina: Meck Mexmie (mchezaji, kapteni)
Maoni: Tumejitahidi sana kucheza lakini game haikuwa yetu, Mungu hakupenda, tunawaomba Watanzania waelewe hilo, tunashukuru kwa sapoti yao.
Mungu hakupenda tushinde - Stars

Jina: Ivo Mapunda (golikipa)
Maoni: Kwanza nawashukuru Watanzania kwa ushiriano wao, ila napenda wafahamu kwamba mchezo ndiyo ulivyo, kuna kufungwa, kushinda na kudroo. Watanzania wasikate tamaa bado tunaweza kufanya vizuri katika mashindano mengine.


Jina: Ally Bushiri (Kocha msaidizi Stars)
Maoni: Vijana wamecheza vizuri, lakini ndiyo mchezo, kuna kufungwa, kudroo na matokeo mengine hatuna budi kukubaliana nayo.

TAIFA STARS YAWALIZA WA TZ!

Abdi Kassim, ( kulia) akila sahani moja na mchezaji wa Msumbiji, ni mshike!
Hata makocha wetu walikuwa na matumaini ya ushindi..!
Muda mfupi kabla ya mechi kuanza, Watanzania walikuwa wamejawa na furaha na matumaini ya ushindi!!! (PICHA NA ISSA MNALLY)