Safu hii (Street Version) ilikuwa miongoni mwa mashabiki wengi wa soka waliofurika ndani ya Uwanja mpya wa Taifa ili kuipa faraja Stars ambayo ilikuwa na kibarua kigumu mbele ya Mambas wa Msumjibi, kwa bahati mbaya Watanzania tulikandamizwa na Wamakonde hao bao moja bila majibu.
Baada ya mechi ‘Street Version’ ilisogea karibu na benchi la Stars ili kusikia maoni ya kocha na vijana wetu hao ambao baadhi yao walionekana kutokwa na machozi, pale walipokuwa wakihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari. Neno kubwa kutoka midomo mwao lilikuwa ni ‘Mungu hakupenda tushinde’.
Jina: Meck Mexmie (mchezaji, kapteni)Baada ya mechi ‘Street Version’ ilisogea karibu na benchi la Stars ili kusikia maoni ya kocha na vijana wetu hao ambao baadhi yao walionekana kutokwa na machozi, pale walipokuwa wakihojiwa na vyombo mbalimbali vya habari. Neno kubwa kutoka midomo mwao lilikuwa ni ‘Mungu hakupenda tushinde’.
Maoni: Tumejitahidi sana kucheza lakini game haikuwa yetu, Mungu hakupenda, tunawaomba Watanzania waelewe hilo, tunashukuru kwa sapoti yao.
Mungu hakupenda tushinde - Stars
Jina: Ivo Mapunda (golikipa)
Maoni: Kwanza nawashukuru Watanzania kwa ushiriano wao, ila napenda wafahamu kwamba mchezo ndiyo ulivyo, kuna kufungwa, kushinda na kudroo. Watanzania wasikate tamaa bado tunaweza kufanya vizuri katika mashindano mengine.
Jina: Ally Bushiri (Kocha msaidizi Stars)
Maoni: Vijana wamecheza vizuri, lakini ndiyo mchezo, kuna kufungwa, kudroo na matokeo mengine hatuna budi kukubaliana nayo.
No comments:
Post a Comment