Tuesday, January 22, 2008

ULIZA SWALI LINGINE !



Rais wa Tanzania katika mapumziko yake ya kila Christmas alipokwenda nyumbani kwake huko Masasi, Mkoani Mtwara kwa ndege ya Serkali alizuru mojawapo ya Day Secondary Schools za hapo mjini na kutoa fursa kwa Wanafunzi kumwuliza maswali yo yote.

RAIS: Nani atafungua dimba?


MASUMBUKO: Viongozi wa Serkali na wa Vyama vya Siasa wanatuambia kuwa Serkali ya Tanzania HAINA DINI. Lakini mbona ofisi zote za Serkali zinafungwa na Wafanyakazi wote Serkalini wanalazimika KUPUMZIKA KILA JUMAPILI?


RAIS: Uliza swali lingine.


MASUMBUKO: Swali la nyongeza; Hivi ni kweli nayo JUMAMOSI ilipitishwa Bungeni iwe pia siku ya mapumziko minajili ya KUWAWEZESHA NA WASABATO wapumzike?


RAIS: Mtoto mwingine?


CHAUSIKU: Katika Awamu ya Tatu kitabu maarufu kiitwacho "MWEMBECHAI Killings and the Political Future of Tanzania" kilipigwa marufuku kuuzwa na kuingizwa humu Nchini na hadi leo hakiruhusiwi kuonekana. Kisa? Tunanong'onezwa kuwa eti ni kwa sababu Kitabu hicho kinawakashifu mashabiki wazawa wa pale "MWEMBE-YANGA", Temeke - hiyo ni sahihi?


RAIS: Na swali la lala-salama nani atauliza?


CHAUSIKU: Hapa nchini Makanisa yote yana Makao Makuu (Headquarters) nje ya Tanzania na yanaletewa misaada ya hali na mali mda wo wote na miaka yote tokea Ukoloni .


Kulikoni misaada ya pesa inayoletwa kuboresha au kujenga Misikiti upya (ambayo maskini kuli hali mingi ni ya udongo na nyasi) INAZUIWA - kunradhi Mhadham Rais, eti ni kutokana na Madrassah zinazoendeshwa humo zinaeneza 'ugaidi'?


BREAKING NEWS!!

Inasemekana Masumbuko na Chausiku 'wametoweka' nyumbani kwao siku ile ile waliporejea kutoka shuleni na 'kuchukuliwa' na watu wanaodhaniwa ni 'Makachero' na mpaka sasa hawajulikani walipo!

JUMANNE KISHOKAH,
DAR ES SALAAM
TANZANIA

4 comments:

Anonymous said...

mrisho nadhani unatakiwa kwenda shule.mambo hayo ni ya kijiweni

Anonymous said...

Una maswali mengi.
Hebu kaka zangu sasa tafadhali chambua ukweli huu.
Kumbuka kaka wataalamu wa dunia hii ni hatari. Utadhani kuwa ubadhilifu na ufisadi wote uko hapo tza tu, lakini ukweli ni kwamba umeenea kote. Waenezao haya ni wachache tu duniani. Na haya yalianza zamani.
Ingia website hizi uone.
http://judicial-inc.biz/slave_traders_.htm,
http://judicial-inc.biz/b.lood_diamonds.htm,
http://judicial-inc.biz/J_oran_va_der_sloot_supplement.htm,
http://judicial-inc.biz/thersea_heinz_kerry_bio.htm,
http://judicial-inc.biz/1.osephardim_of_curacao.htm,
http://judicial-inc.biz/j_history_caribbean_jews.htm,
http://www.blacksandjews.com/Jews.of.Black.Holocaust.ag.html,
http://sunray22b.net/slavery.htm,
www.jewwatch.com, www.erichufschmid.net, www.iamthewitness.com, www.prothink.org.

Anonymous said...

...kweli kabisa atafute habari za kuleta hapa sio kukaa na kuchochea siasa za kidini!maana habari yote inalenga kwenye udini mtupu!mambo ya kenya unayaona lakini ukabila unavyowatesa!??wanauana tu kila sasa!kwa habari yako hiyo watu wakuelewe una nia gani??kugombanisha watu wenye imani tofauti??kumfananisha raisi na cheo cha kiongozi wa kanisa una maana gani???si uchokizi kabisa huo!ingawaje wewe umeletewa habari lakini unatakiwa usome kwanza na ujue kuwa wasomaji wako wataipokea vipi ukijua kuwa wasomaji wako wanatoka katika imani tofauti!zaidi ya hapo utuambie kuwa hii blog yako ina upande ambao unaegemea zaidi!mambo ya kijiweni yaishie huko huko sio kuleta mahali kwenye watu wenye imani tofauti!utaleta mgongano kwa watu wakati Tanzania yetu tunaijua ni nchi yenye amani.

Anonymous said...

Kama msimamo wako ni huo wa kichochezi bwana mrisho anzisha blog ingine ya mambo hayo utapata watu wa aina hiyo. Au kama unaashiria kuwa hii blog sasa ndo unataka iwe hivyo, kuna watu utakaobaki nao hapa. Lakini nakuasa tu si jambo zuri hili unaloshabikia. Hizo siku za kupumzika za wikiendi nchi nyingi duniani ambazo hazina dini wanapumzika siku hizo hizo, ni utaratibu tu uliokubalika kama kuendesha gari kulia au kushoto. Hayo ya Mwembechai tumesikia hadithi nyingi hadi tumechoka, nayo yamebakia huko yalikobakia. Ningekuwa mimi mmojawapo wa waathirika wa hiyo Mwembechai kama kweli nilikuwa na ushahidi wa kufanyiwa njama/hujuma ningekwenda mahakamani na nina uhakika ningepata haki (ona mke wa Kombe alifidiwa sh mil 300 baada ya mumewe kuuawa na polisi kimakosa. Lakini angekaa kimya tu kunung'unika kichinichini au kwenye majukwaa zingetoka wapi? Tungebakia tu na hadithi za kubahatisha. Lakini sasa tuna ukweli wa yaliyotokea maana ushahidi wote ulianikwa mahakamani).

Kwa hiyo ndugu zanguni tuacheni siasa hizi za kichochezi (hii wala si dini inayojadiliwa hapa). Hazitatusaidia lolote, na badala yake zitafanya maisha yetu yazidi kuwa magumu.