Monday, January 21, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Makamua: Nimewahi kutongozwa na jimama, tena mwenye nyadhifa zake.

Kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa, 'Hot Corner' ilikutana uso kwa uso na staa wa Bongo, Mack Paul Sekimanga a.k.a Makamua, tofauti na siku nyingine ambapo hupiga stori na watu maarufu kwa njia ya simu.

'Dogo' akiwa ni mwanafunzi katika Sekondari ya Makongo, Dar es Salaam ambaye pia anafanya kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii kupitia sanaa ya muziki wa kizazi kipya, alikutana na maswali 'hot' kutoka kwa mwandishi Catherine Kassally.


1. Kwa nini unajiita Makamua?

Kwasababu nilijigundua ninauwezo mkubwa wa kukamua, namaanisha kuimba, kitu kilichowafanya washikaji zangu pia waniite hivyo.

2. Nani aliyefanya kazi kubwa ya kukuinua mpaka leo uko juu katika game?

Yaani nawashukuru sana wazazi wangu japo siku za mwanzo walikuwa wananibania, lakini baada ya kuona matunda yangu kila mmoja ananipa sapoti ya kutosha hasa mama yangu mzazi nampenda sana.

3. Inasemekana unauhusiano wa kimapenzi na msanii Enika. Je, hilo linaukweli?

Makamua: Inawezekana mimi kutembea na Enika, kwani ni mtoto wa kike mwenye mvuto hasa kwangu, sijui nieleze vipi. Ila napenda mjue namzimia kuliko maelezo.

4. Ulishawahi kutongozwa na jimama (shugamami) yoyote?
Ndiyo, niliwahi kutongozwa na shugamami tena mwenye wadhifa mkubwa serikalini, lakini nilimchomolea kwasababu napenda kuwa na rafiki au mchumba wa rika langu.

5. Kama ukijaaliwa kuwa na familia yako ungependa kuwa na watoto wangapi na uzae na mwanamke wa aina gani?

Ningependa kuwa na watoto wawili, si unajua maisha yanabana sana, pia ningependa kuzaa na mwanamke ambaye ananiheshimu, anajiheshimu yote hayo yanawezekana kwa mwanamke ninayempenda.


Madee Kuomba msamaha

Baada ya kunusurika kupigwa na mashabiki katika baadhi ya shoo alizofanya hivi karibuni, pale alipoimba wimbo wake 'Hip Hop haiuzi' msanii Hamad Ally 'Madee' kutoka ndani ya Familia ya Tip Top Conection, yenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam yupo katika ziara ndefu akiwaomba mashabiki hao wamuelewe, Violet Mushi alipiga naye stori.

Akipiga stori na Abby Cool & MC George Over The Weekend, kwa njia ya simu msanii huyo ambaye hivi sasa yuko Kanda ya ziwa akiendelea na ziara hiyo alisema kwamba anachojaribu kufanya ni kuwaomba mashabiki waelewe vitu alivyoimba kunako traki hiyo.

"Watu wamekuwa wakiupokea wimbo huo katika fikra potofu, kitu ambacho kinaniweka katika wakati mgumu, ndiyo maana nataka kuwaelimisha kwamba mimi kama msanii nimefikisha ujumbe ili ufanyiwe kazi, nilichofanya ni kukusanya mawazo ya mashabiki mbalimbali na kuyatungia wimbo, siyo kama nilikurupuka nikarekodi wimbo huo, mbona mimi pia nafanya Hip Hop?', alihoji Madee.

Mpaka sasa msanii huyo ambaye pia baadhi ya kazi zake zinapatikana ndani ya albamu ya Tip Top Compiration yenye mchanganyiko wa kazi za wasanii wa familia hiyo, ameshazunguka sehemu kibao Tanzania Bara ikiwemo Singida, Nzega, Kahama, Musoma, Kigoma, Mwanza na kwingine akiwa na wakali wengine kama PNC na Kassim kwa ajili ya shughuli hiyo.
Tollywood kuisapoti muvi ya Imbwiga

Kampuni ya Tollywood ya Dar es Salaam ambayo inakuja juu katika tasnia ya usambazaji wa muvi Bongo, imejitolea kuisimamia filamu kali na ya kutisha, Imbwiga inayotarajiwa kudondoka mtaani hivi karibuni.

Stelingi wa muvi hiyo, Majani Kasoga Nsyuka, aliyepata kutamba ndani ya filamu ya Nsyuka, ameiambia safu hii kwamba, ubora wa kazi hiyo ndiyo umemfanya apate shavu Tollywood na kwamba ana uhakika ataliteka soko la Bongo.

"Kwa wale mashabiki waliopata kuniona kwenye filamu ya Nsyuka, watakubaliana na mimi kwamba nimekuja tofauti sana. Ndani ya muvi hiyo nimecheza sehemu tatu tofauti, yaani Imbwiga ambao ni mzimu wa watu wa Musoma, Bob Kijiti ambaye ni kijana wa mtaani na Majani mzimu wa Kijiti," alisema.

Aidha ndani ya muvi hiyo mashabiki watapata fulsa ya kushuhudia vitu vipya kabisa katika sanaa ya filamu Bongo ikiwemo ile sehemu ambayo Bob Kijiti amecheza kama Majani, yaani mtu mmoja ambaye anaonekana kama watu wawili tofauti. Kwa kifupi ni bonge la picha ambalo wewe msomaji na shabiki wa filamu za Kibongo hutakiwi kulikosa.

No comments: