Wiki iliyopita tuliendelea na sehemu ya pili ya makala haya kwa kuangalia umuhimu wa maji katika mwili wa binadamu. Leo tunaendelea kwa kuangalia umuhimu wa mwanga wa jua na hewa katika suala zima la binadamu kuwa na afya bora…
Tumeona ni kiasi gani maji ni muhimu mwilini na mwili ambao hauna maji ya kutosha unapata matatizo kiasi gani. Ni aibu kwa mtu kumaliza siku nzima kwa kunywa glasi moja tu ya maji au bila kunywa maji kabisa. Ni hatari pia kuwa na tabia ya kunywa maji pale unaposikia kiu, kama kweli unajali afya yako na unaogopa maradhi, yaheshimu maji kuliko kitu kingine.
2. MWANGA WA JUA
Vitamini ni miongoni mwa virutubisho muhimu mwilini ambavyo humpatia binadamu afya njema. Kwa upande wa vitamini, kuna aina nyingi za vitamini zinazopatikana kwenye vyakula tunavyokula kila siku, lakini kuna vitamini inayopatikana kutokana na mwanga. Hivi umewahi kujiuliza kama kusingekuwa na mwanga kusingekuwa na maisha?
Mungu alimuumba binadamu na kumpa uwezo zaidi wa kuishi sehemu ya nje yenye mwanga kuliko ndani. Kwa mujibu wa imani iliyopo miongoni mwa waumini mbalimbali wa dini, Mungu alimuumba Adam na kumuweka kwenye bustani ya wazi akiwa mtupu ili mwili wake wote upate mwanga wa jua.
Katika uumbaji wake, Mungu ameweka siri kubwa kuhusu jua na ngozi ya binadamu. Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi, kuna maajabu yanatendeka chini ya ngozi ya binadamu pale inapopigwa na mwanga wa jua la asubuhi. Kuna aina fulani ya mufuta inayojulikana kwa jina la STEROLS iliyoko chini ya ngozi ambayo inapopigwa na mionzi ya jua huamsha vitu vinavyojulikana kama ERGOSTEROLS ambavyo huzalisha vitamin D mwilini.
Vitamini D ni ya kipekee, kwani ndiyo vitamin pekee inayojizalisha yenyewe katika mwili wa binadamu kwa kutumia mwanga wa jua. Kwa ngozi ya kawaida, inahitaji dakika 15 au pungufu kuzalisha IU 10,000 hadi 20,000 kwenye mwanga wa jua, hasa la asubuhi.
Inaelezwa kuwa vitamin D ni kirutubisho chenye faida nyingi katika mwili wa binadamu, miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuimarisha kinga ya mwili, kupunguza maumivu ya mwili, kuchangamsha mwili na akili.
Faida zingine za vitamin D itokanayo na jua ni kung’arisha ngozi na kuongeza kasi ya usagaji chakula mwilini na kuchoma kalori kwa wingi hivyo kusaidia pia katika suala zima la kupunguza uzito wa mwili. Aidha vitamin hii hupunguza kolestro mwilini, uhimarisha mifupa na meno na faida nyingine nyingi.
JE, UNAWEZAJE KUPATA FAIDA ZA JUA BILA KUWA KATIKA HATARI YA KUPATA KANSA?
Ili kupata faida za jua na kujiepusha na hatari ya kupata kansa itokanayo na jua, anza kwa kukaa kwenye jua la asubuhi kwa dakika 10-15 kwa kuanika sehemu ya uso, mikono na miguu, kisha ongeza muda hadi dakika 30. Mwili huhifadhi vitamin D mwilini kwa zaidi ya wiki moja. Epuka jua kali na usijikinge na kitu usoni unapoota jua.
Kikubwa zaidi katika kujiepusha na kupatwa na saratani ni kuepuka ulaji wa mafuta yatokanayo na wanyama, ulaji wa vyakula vya kukaanga au vyakula vya kwenye makopo ambavyo vimewekewa kemikali zenye madhara. Mafuta mazuri ni yale ya asili yaliyomo kwenye matunda na mboga kama vile nazi, karanga, korosho, maparachichi, n.k.
3. HEWA
Kitu kingine muhimu katika kutimiza malengo ya afya bora, baada ya maji na mwanga wa jua ni hewa safi. Ni ukweli uliowazi kuwa binadamu anaweza kuishi kwa wiki 5 hadi 6 bila chakula. Anaweza pia kuishi siku chache bila kunywa maji lakini akikosa hewa hufa ndani ya dakika chache tu! Mahitaji muhimu ya mwili kuliko vitu vyote sio virutubisho, protini au mafuta, bali ni hewa safi (Oxygen).
Aina ya hewa tunayovuta, inaweza kuwa na athari katika muonekano wa sura zetu, jinsi tunavyojisikia, jinsi tunavyokabiliana na maradhi na hata umri wa maisha yetu. Ili mwili uwe na damu nzuri, unahitaji kuvuta hewa vizuri na ili mwili uwe katika hali nzuri unahitaji kupata hewa safi na ya kutosha.
Uvutaji wa hewa mzuri huyawezesha mapafu kupata hewa ya oksijeni ambayo husafisha damu na hivyo kusafirisha uhai katika kila sehemu ya mwili. Hewa safi hutuliza mishipa, hutoa hamu ya kula, huboresha usagaji wa chakula na hutoa usingizi mzuri.
Mgonjwa anaweza kupona haraka akiwa katika mazingira yenye hewa safi na ya kutosha na huweza kufa haraka kwa kukosa hewa safi kuliko hata akikosa chakula. Tiba yenye mafanikio zaidi kwa wagonjwa wa kifua kikuu ni kupata hewa safi na ya kutosha usiku na mchana na wanapowekwa kwa muda mrefu nje sehemu yenye hewa safi na ya kutosha hupata nafuu haraka.
Wiki ijayo tutazungumzia kwa undani umuhimu wa hewa ambayo kila sekunde tunaitumia!

1 comment:
Mkuu, shukrani za pekee kwa mchongo wako katika afya yetu. Ninaye rafiki yangu anasumbuliwa sana na GAUTi, tayari kaanza pata uvimbe katika kiwiko chake cha mkono wa kushoto na kidole kikubwa cha mguu nacho kimemvimba. Tutashukuru sana kama utatupatia maoni na ushauri wako juu ya tiba yake. Stay blessed.
Post a Comment