Jide awavutia mastaa kibao
Msanii ‘mbishi’, anayefanya vyema kunako game ya muziki wa kizazi kipya na bendi yake ya Machozi, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’, hivi karibuni amekuwa kivutio kikubwa kwa mastaa kibao, hasa wa muziki wa Bongo Flava, Amina Salim anakupa ishu kamili.
Safu hii ambayo ni miongoni mwa wapenda kujiachia ndani ya Ukumbi wa Zhonghua Garden uliyopo maeneo ya Moroco Dar es Salaam, ilishuhudia mastaa hao wakijiachia kila siku ya Ijumaa, Jide anapokuwa kazini na bendi yake katika ukumbi huo.
“Yaani hapa sisi ni kama kijiwe, hii yote ni kwa ajili ya kumsapoti mwenzetu kwa kukubali anachofanya, ni kazi nzuri ndiyo maana hata sisi tunapata nguvu na moyo wa kuja hapa kama unavyoona tumejiachia, “alisema Chidi Benz akiwa ndani ya ukumbi huo mwishoni mwa wiki iliyopita.
*******************************************************************
Sheila ampindua Lucille
Baada ya chakula cha usiku wa juzi, baadhi ya washiriki ndani ya Jumba la BBA waliamua kupata ‘chocolate’, lakini Takondwa ‘TK’ na Sheila walionekana wako kushoto kabisa na vitu vitamuvitamu kama hivyo, badala yake walionesha kuwa na hamu ya kuvuta sigara.
Mrembo Sheila ndiye aliyeonesha zaidi kuhitaji sigara na kwamba bila kiburudisho hicho hawezi kuendelea kuwemo ndani ya jumba hilo, tabia ambayo imemfanya awe na ubavu wa kumpindua Lucille kwa ‘TK’ ambaye pia ni mpenda ‘fegi’.
Baadhi ya mashabiki wa shindano hilo, kupitia maoni waliyotuma mtandaoni wameonekana kumsikitikia Lucille ambaye amepigwa chini na ‘TK’, mwanaume ambaye alianza naye uhusiano.
Hata hivyo, watu wengi wanasapoti ukaribu wa Sheila na TK kwani mambo yao yameonekana kushabihiana kama hilo la kuvuta sigara.
BBA: Latoya,Morris sasa ni kama mke na mume
Mwanzo yalionekana kuwa ni mapenzi ya rasharasha, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda, ukaribu unakuwa wa kutosha zaidi kati ya Latoya Lyakurwa wa Bongo na Morris Herbert Mugisha wa Uganda ambao sasa wanaonekana kama mume na mke ndani ya Jumba la BBA.
Ishu iliyopo kwa wapenzi hao hivi sasa ni ushirikiano wa kutosha, ikiwemo kulala pamoja na kubadilishana mawazo kama ilivyokuwa katikati ya wiki hii ambapo Latoya akiwa kifuani kwa Morris alimwambia kuwa, ameikumbuka sana simu yake ya mkononi kitendo ambacho kilimshitua Mganda huyo ambaye alimuuliza kwa nini ameikumbuka simu na ndani ya simu hiyo kunani?
“Nimekumbuka nyumbani, simu ni kampani yangu kubwa maishani mwangu,” alijibu Latoya akiwa amekumbatiwa mikononi na Morris.

Ijumaa KIng of Hip Hop Mmoja kutoka wiki ijayo
Wakati wasomaji wako bize kutuma kura zao ndani ya shindano la Ijumaa King Of Hip Hop ili wajihakikishie kuondoka na zawadi ambazo zimetangazwa hivi karibuni, mshiriki mmoja kati ya saba waliyobaki shindanoni atatolewa wiki ijayo.
Mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso, alisema na ShowBiz kwamba, mshiriki mmoja ilikuwa atoke Ijumaa ya leo lakini kutokana na idadi ya kura zilizotumwa kuwa nyingi, imebidi wasogeze mbele ili wapate nafasi ya kuzihesabu kwa umakini zaidi.
“Mpaka sasa tumebaki na washiriki saba ambao ni Kalapina, Prof. Jay, Fid Q, Chid Benz, Lord Eyez, Johmakini na Langa aliyerudishwa hivi karibuni. Bado tunaendelea kupokea kura za wasomaji na wapenzi wa Hip Hop ambao ndiyo majaji wa shindano hili, kwani bila wao hakuna kitakachofanyika,” alisema Mateso.
Mateso aliwakumbusha wasomaji jinsi ya kupiga kura katika shindano hilo. “Wanaandika neno HP, wanaacha nafasi, wanaandika jina la mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi, kisha wanatuma kwenda namba 15551,” alisema Mateso.

No comments:
Post a Comment