Akiwa mapumzikoni Bongo, akila ‘bata’, baada ya kuwa bize na kitabu nchini Uganda, msanii, Khadija Shabani ‘K-Sher’ alisema na safu hii kwamba hakuna kitu kinachomkera na kumharibia stimu kama tabia ya watu wanaopenda ‘kubipu’ katika simu yake.
Akipiga stori huku akiwa na jazba ya kutosha binti huyo anayefanya kazi zake kupitia familia ya Tip Top Connection alisema kwamba, muda mwingi amekuwa hapati usingizi wa ukweli, kwasababu ya makele ya simu yake ambayo inabipiwa usiku kucha na watu asiowafahamu.
“Yaani hawa watu sijui hawana kazi ya kufanya, wengine wanapiga, ukiwauliza shida hawaongei kitu zaidi ya kukata simu, wanaobipu na meseji ndiyo usiseme. Kama ni mashabiki wangu, nawaomba sana wawe wananipigia mchana na siyo kupibu au kutuma meseji mbaya,” alisema K-Sher.

****************************************************
BBA III:Latoya, Lucille ngoma droo!
Na Hamida Hassan
Ikiwa ni siku ya nane tangu waingie ndani ya Jumba la Big Brother Africa III, washiriki wawili, Latoya Lyakurwa kutoka Bongo na Mnamibia Lucille Naobes wameoneokana kushindana na pengine kutoka ‘droo’ (sale) kwa vitendo vyao vya ngono ambavyo wamekuwa wakifanya ndani ya jumba hilo bila ya kuwa na staha ukizingatia kwamba ni mapema mno toka walipoingia kunako jumba hilo.
Mara ya kwanza Latoya alionekana kuongoza kwa vitendo hivyo ambapo alikuwa akiwaniwa na vijana wawili, Ricco kutoka Angola na Morris kutoka Uganda ambaye ndiye aliyeibuka na ushindi, hivi tunavyoongea tayari anaumiliki ‘mzigo’ wa Kibongo.
Kwa upande wa Mnamibia Lucille, naye ameona njia rahisi ya kujipatia mkwanja unaoshindaniwa katika jumba hilo ni kufanya ‘malove dave’ na mshiriki wa Zambia, Takondwa a.k.a TK ambapo walionekana laivu wakipeana mate huku TK akiwa amezidiwa na hisia kuonesha kwamba alikuwa akifurahia kile kilichokuwa kikitendwa na Luccile.
Mashabiki wa mchezo huo, wameonekana kushabikia penzi la Morris na Latoya huku wakidai kuwa inawezekana huu ukawa uhusiano rasmi kama ulivyokuwa kati ya Richard na Tatiana ambapo wamefikia hatua ya kuwabatiza jina kwa kuwaita Morislat kama wanavyotoa maoni wasomaji kwasababu ya matendo yao ambayo yameanza mapema.

********************************************************
KING OF HIP HOP Kumekucha
Wakati zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuwatafuta washiriki watano watakaoingia fainali likiendelea, waandaaji wa shindano la kumtafuta Ijumaa King Of Hip Hop wamezitaja baadhi ya zawadi zitakazokwenda kwa wasomaji au wapenzi wa Hip Hop watakaotuma kura nyingi zaidi, kitendo kinachoashiria kwamba, sasa kumekucha.
Mratibu wa mpambano huo, Charles Mateso, ndani ya safu hii alitamka kwamba zawadi hizo ambazo ni meza ya kisasa kabisa kwa ajili ya kupamba sebuleni pamoja na fulana zitaanza kutolewa siku chache zijazo, huku nyingine kibao zikiendelea kuandaliwa.
“Bila wasomaji au wapenzi wa muziki wa Hip Hop kutuma kura zao, hatuwezi kufanya kitu ndiyo maana tumeamua kuwapa kipaumbele kwa kuwaandalia zawadi hizo kama motisha kwa mchango mkubwa wanaoutoa katika shindano hili.
Washiriki waliobaki shindanoni ni Kalapina, Prof. Jay, Fid Q, Chid Benz, Lord Eyez, Johmakini na Langa aliyerudishwa hivi karibuni. Tunawaomba wasomaji waendelee kutuma kura zao kwa kuandika neno HP, wanaacha nafasi, wanaandika jina la mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuwa mshindi, kisha wanatuma kwenda namba 15551,” alisema Mateso.

*****************************************************
STREET VERSION:
STREET VERSION:
No comments:
Post a Comment