Friday, December 19, 2008

BURIANI SHUJAA HENRY!

Mhariri mkuu wa Channel Ten, Dina Chahali, akipita mbele ya jeneza la marehemu kutoa salamu zake za mwisho wakati wa kumuaga mfanyakazi mwenzao Henry Makange.
Jeneza la marehemu 'shujaa' henry makange, ambaye alikuwa mfanyakazi wa kituo cha televisheni cha channel ten aliyefariki kwa ajali akielekeza kazini jumatano iliyopita. mchana wa leo mwili wake umeagwa kwa heshima zote na ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake na majirani nyumbani kwa mkewe oysterbay jijini dar es salaam. Marehemu amesafirishwa kwenda kibaha kwao kwa maziko kesho mchana. henry atakumbukwa kwa mengi, kikubwa ni jinsi alivyonusurika katika ajali ya gari alimokuwamo shujaa mwezake Athuman Hamis miezi miwili iliyopita, ambaye aliumia mgongo na sasa yuko Afrika kusini akiendelea na matibabu, yeye ndiye aliyeokoa maisha ya mwenzake..mungu ametoa na mungu ametwaa, ailaze roho yake peponi AMIN!

Uncle hashim wa miss tanzania akitoa salam zake za mwisho kwa marehemu.
Mke wa marehemu, Jane, aliyeolewa mwezi mmoja tu uliopita, akimuaga mumewe kwa uchungu kabla ya kuelekea kibaha kwa maziko
Mke wa marehemu akiwa amemkumbatia mwanae, Melan, aliyezaa na marehemu wakati akisoma sala ya mwisho kwa kipenzi chake Henry. Kulia ni Salum Mwalimu, mtangazaji wa Channel Ten akimsaidia mfiwa.

No comments: