Saturday, December 20, 2008

WIKI YA MAJONZI!

Ilikuwa ni wiki ya majonzi kwa AY ambaye alifiwa na mama yake mpendwa Lyidia ambaye amezikwa leo katika makaburi ya Kindondoni jijini Dar....Mungu awape moyo wa subira wafiwa na amrehemu mama yetu Lyidia Yessaya- Amin!
Prof Jay akimuombea marehemu baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la mama yake AY.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Said Kalembo, akitoa nasaha kwa wafiwa katika msiba wa mamake AY..Kalembo aliwahi kuishi jirani na familia ya AY walipokuwa Mororgoro miaka ya nyuma
Ilikuwa ni wiki ya majonzi pia kwa famila ya Herry Makange ambaye amezikwa leo mjini Kibaha....na haya ndiyo makazi yake ya milele!
Jane, mke wa marehemu Herry akitupia mchanga kwenye kaburi la marehemu mumewe mjini Kibaha alikozikwa...Mungu alitoa na Mungu ametwaa..jina lake lihimidiwe!

2 comments:

Anonymous said...

Hapo msibani hakuna wakina mama...iweje Jane ashikwe na kina kaka?

Anonymous said...

Hapa ndo wasanii wa kibongo wanapo chemsha...msibani unaenda umevaa kaptura?? Prof Jize umechemsha mkubwa...nilifikiri ni muungwana wa kuweza kutofautisha matukio na haiba esp wewe ulipewa nafasi muhimu ya kuwakilisha wasanii wenzio lkn umeshindwa, muone Mh Kalembo amepiga suti wewe umezidi kuupotosha umma ili waendelee kuamini kwamba wasanii ni wauni tu... nimekudis value kwa hilo.