Monday, October 6, 2008

MAXIMO ATUA ZIZZOU FASHION

Juzi Ijumaa kocha mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo alifanya Shopping katika duka la nguo maarufu jijini Dar es salaam, Zizzou Fashion lililoko Sinza jijini Dar es salaam kama anavyoonekana katika picha hizi.
...akiingia Zizzou Fashion Store
....akitafakari cha kununua na pembeni yake, mmiliki wa duka hilo, Tipo Athuman.
...akijaribu fulana ya Taifa Stars...
...hii bomba..
Kocha Maximo akiangalia aina mbalimbali za raba zilizopo Zizzou Fashion
Kocha Maximo akiwa na Mmiliki wa Zizzou Fashions Stores, Athuman Tippo.
Ilikuwa zali la mentali kwa masela wa Sinza Africa Sana kukutana na Maximo, hivyo kuomba kupiga nae picha!
Tipo akionekana kufurahia jambo wakati alipokuwa na kocha Maximo kwenye bustani za Atrium Hotel zilizopo jirani na Zizzou Fashion.

EE BWANA DAH Mariah Carey!!



Unaweza usiamini, lakini huu ndiyo ukweli kwamba staa wa muziki wa R&B, Maria Carey kabla hajafunga ndoa na kijana Nick Cannon hivi karibuni, aliwahi ‘kujilamba’ (kutoka faragha) na midume zaidi ya kumi kwa nyakati tofauti.

Kwa mujibu wa mtandao wa ‘intaneti’ kati ya wanaume wote aliowahi kufanya nao mapenzi, ni wawili tu ndiyo aliyofanikiwa kufunga nao ndoa, Tommy Mottola (1990) na Nick Cannon aliyejitwisha mzigo mapema mwaka huu.

Kila kukicha baadhi ya mashabiki na watu wa karibu wa mastaa hao wanazidi kuitabiria ndoa yao kifo kutokana na tabia ya Mariah kutopenda kutulia na mwanaume mmoja ambapo siku kadhaa zilizopita watu wengi walishangaa baada ya kuwaona wawili hao wakiwa pamoja, kwani walitegemea kusikia kwamba, siku chache baada ya ndoa yao, Mariah Carey na Nick Cannon wameachana.

Kupitia safu hii ‘Ebwana dah!’ itakuwa inakudondoshea ishu za mastaa mbalimbali wa kiwanja kuhusiana na maisha yao ya uhusiano. Unachotakiwa kufanya wewe msomaji ni kutuambia unapenda kujua nani aliwahi kuwa na uhusiano na nani? Tutumie ujumbe mfupi kupitia simu namba +255 715-110 173 au Wikienda@globalpublisherstz.com **************************************************

WIKIENDA SHOWBIZ!


Fella: Siyo umeneja tu, hata stejini nimo
Kiongozi wa kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Family kutoka pande za Temeke, Said Fella a.k.a Mkubwa hivi karibuni aliwaonesha mashabiki wa kundi hilo kuwa yeye siyo kiongozi wa maneno tu, hata stejini anakamua pia.

‘Mkubwa’ alijitosa stejini na kushambulia jukwaa na ‘wanae’ (kama anavyoonekana pichani katikati) huku akishangiliwa na mashabiki kibao waliofurika ndani ya Ukumbi wa Dar West Park Tabata, Dar es Salaam wakati kundi hilo lilipokuwa linasababisha bonge la shoo kwaajili ya kusheherekea Sikukuu ya Idd.

‘Mara nyingi huwa napanda stejini kuwahamasisha ‘wanangu’, siunajua muziki ndiyo ajira yetu? Huwa wanafurahi sana ninapofanya hivyo, wanajikuta wakiongeza kasi ya kutosha,” alisema Fella.
'3 bila Rimiksi' bila Inspector, Kalama, Why?
Uvumi wa wasanii wawili, Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’ na Kalama Salum Jongo ‘Luteni Kalama’ kujitoa ndani ya kundi la TMK Halisi ulianza kuenea taratibu, baadae ukafikia hatua kwa wasanii hao kutamka hadharani kupitia baadhi ya vyombo vya habari, Rebeka Benard anadondoka nayo.

Lakini kwa upande wa kiongozi wa kundi hilo, Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ bado hakubaliani na hilo kwa kukanusha kuondoka kwa wasanii hao au kukataa kulizungumzia, kitu ambacho kinaonekana kuwachanganya wapenzi wengi wa kundi hilo.

Sisi kama wadau wa mradi huo tunauliza, mbona kunako rimiksi ya ngoma yenu, Tatu bila sauti za Inspector na Kalama hazimo, badala yake tumesikia sauti mpya ya msanii anayejiita Baba Levo. Why?
******************************************************************************

Friday, October 3, 2008

IJUMAA SHOWBIZ

Fiesta 2008:Mashabiki wa Tanga kujiachia kesho
Lile tamasha kubwa la burudani, linalowakutanisha mastaa kibao wa muziki wa Kizazi Kipya, linalokwenda kwa jina la Fiesta linaloandaliwa na Prime Time Promotion, limerejea tena ambapo shoo ya ufunguzi itafanyika kesho, Oktoba 4, 2008 jijini Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.

Akichonga na kona hii katikati ya wiki Mratibu wa shoo hiyo Hamis Mandi a.k.a B 12, amesema shoo ya mwaka huu si ya kitoto na kwamba Tanga wajiandae kupata burudani ya ukweli kutoka kwa wakali wa Bongo Fleva.

“Ebwana shoo ya mwaka ina maandalizi ya kutoka mtu wangu, yaani ninachoweza kusema ni kwamba mashabiki wajitokeze kwa wingi hapo kesho, maana kutakuwa na mawe ya maana mzazi...” alisema B 12.

B 12 alisema wameamua kufanya shoo ya ufunguzi jijini humo kwasababu mwaka jana, Tanga ndiyo mkoa ulioongoza kufurika maashabiki wengi zaidi kuliko sehemu nyingine.

“Mwaka jana kulikuwa na nyomi si ya kitoto, na hii ndiyo sababu tukaamua kuanza nao mwaka huu. Tunafanya hivyo kama zawadi kwako namara zote huwa tunafanya shoo ya ufunguzi katika mwaka unaofuata mahali ambapo mwaka jana mashabiki walihudhuria wengi zaidi,” alisema B 12.

“Kila wakati huwa tunafanya kweli lakini mwaka huu tumedhamiria kufanya zaidi ya ukweli, tunachoweza kusema sisi kama Prime Time Promotion ni kwamba kiu za mashabiki zitakatika, yaai watafurahia sana shoo ya mwaka huu,” alisema.

Wakali watakaoonyesha cheche kesho ni pamoja na Profesa Jay, Ay, Ray C, QJ, Q Chief, Dully Skyes, Matonya, Wanaume Halisi, Wanaume TMK, Mwasiti, Marlow, Chid Benz, Mangwea, Jose Cameleon, Nyota Ndogo na wengineo.

Wakati mwaka jana kauli mbiu ilikuwa Boda 2 Boda, mwaka huu washkaji wamekuja na JIRAMBE, kwanini wamesema hivyo? Huyu hapa B 12 anafafanua; “Kaka chochote cheye utamu lazima ujirambe, kwahiyo makamuzi ya mwaka si ya kitoto kiasi kwamba lazima mashabiki watajiramba, ndiyo maana tukatumia kauli mbiu hii.”

***********
Jay Dee ndani ya Kora tena!
Kwa mara nyingine tena Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee, amepata shavu la kwenda kuiwakilisha Bongo katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Kora zitakazofanyika Disemba mwaka huu, Tanapa, Nigeria.

Katika tuzo hizo Jay Dee anashindanishwa katika category ya kuwania Tuzo ya Mwanamuziki Bora kutoka Afrika Mashariki kupitia kibao chake kikali kinachokwenda kwa jina la Shukrani.

Katika category hiyo Jay Dee au Komando atachuana vikali na wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki ambao ni Nameless, Valerie Kimani na Wahu kutoka Kenya na Klear Kut, Michael Ross na Blu 3 wa Uganda.

kama Jay Dee atajinyakulia tuzo hiyo, atakuwa na uhakika wa kuchota kiasi cha dola milioni moja za Kimarekani ambazo kwa pesa ya madafu ni sawa na shilingi bilioni moja. Kazi kwako Bi dada, utuletee ushindi huo nyumbani.
Janet:Sasa nipo shwaari kabisa!
Mwimbaji machachari katika Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Janet Isinike, amesema kwamba kwa sasa hali yake ni shwari kabisa baada ya kutokuonekana jukwaani kwa majuma kadhaa kutokana na matatizo ya kufanyiwa upasuaji wa uvimbe uliyokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu. Rhobi Chacha anakupa ishu kamili.

Katika mahojiano maalum na ShowBiz wiki iliyopita, Janeth alisema anamshukuru Mungu baada ya afya yake kutengemaa na amshabiki wake wakae mkao wa kuburudishwa na sauti yake ambayo alidai kwamba anaiamini.

“Nina furaha kubwa sana kupanda jukwaani kwani kwasasa ni mzima wa afya njema na matarajio yangu ni kuongeza bidii zaidi na ninachoweza kuwahakikishia mashabiki wangu ni kwamba wajiandae kupata vitu vya uhakika kutoka kwangu,” alisema.

Aidha alisema kuwa, kukaa kwake kwa muda mrefu bila ya kupanda jukwaani kumempa akili ya kutunga wimbo mpya ambao utatambulishwa hivi karibuni ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wote wa Twanga Pepeta.

************
Fainali za kumsaka mkali wa rapu zapamba moto!
Shindano la kumsaka mkali wa rapu katika muziki wa Dansi, limefikia patamu baada ya waandaaji wa mtanange huo kutangaza siku ya fainali na zawadi za ya mshindi wa kwanza. Issa Mnnaly anashuka nayo.

Mmoja wa waratibu wa shindano hilo anayekwenda kwa jina la Emanuel Likunda aliliambia Ijumaa kwamba fainali za mchuano huo zitafanyika Ijumaa, Oktoba 10, 2008 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kwamba zawadi ya mshindi wa kwanza ni gari aina ya Toyota RAV 4.

“Tunaamini ili burudani yoyote iwe nzuri ni lazima kuwe na mashindano, kadhalika ili shindano liwe zuri ni vyema kukawekwa zawadi nzuri, hii ndiyo sababu iliyotufanya tuamue kutoa zwadi ya gari RAV 4 kwa ajili ya kuwapa motisha marapa wa bendi zetu,” alisema Likunda.

Katika fainali hizo, marapa watakaotoana jasho ni pamoja na Kalala Junior, Khalid Chokoraa (African Stars Band, pichani juu) Papii Katalog, Seven na Toto Kalala (FM Academia) Greyson Semsekwa na Juakali (T. Respect) na Kanal Top wa Akudo Impact.
************

Bahati Nasibu ya Jishindie Benz Yapagawisha mashabiki mitaani!


Ikiwa ni siku chache tangu kuzinduliwa kwa Shindalo la Jishindie Benz, linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd ya jijini Dar es Salaam, wasomaji wameonekana kupagawa baada ya kugombania magazeti na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.

Gari la matangazo la kampuni hiyo ambalo hupita kila kona ya jiji la Dar es Salaam, limekuwa likizingirwa na wasomaji wakitaka kununua vitu mbalimbali vinavyozalishwa na Global Publishers. Washkaji changamkieni tenda hiyo, huwezi jua mshindi anaweza kuwa wewe.

Wednesday, October 1, 2008

UNATAKA KUPUNGUZA UZITO? SOMA HAPA!


BAADA ya kupata maswali mengi kutoka kwa wasomaji wetu kuhusu jinsi ya kupunguza uzito, leo nimeona nirejee makala haya kwa kina ili wale wenye kiu ya kupunguza ama kuongeza uzito waweze kukata kiu yao kwa kupata somo hili muhimu kwa afya zao.

Inapaswa kukumbukwa kwamba suala la kupunguza uzito linahitaji nia, uvumilivu na uelewa wa vyakula unavyokula. Watu wengi wanafikiri kupunguza uzito ni kupunguza kula tu au kufanya sana mazoezi.

Hatua ya kwanza unayopaswa kuchukua kabla ya kuamua kupunguza ama kuongeza uzito wako ni kujitambua hali yako ya mwili na kilo ulizonazo. Unapaswa kujua urefu wako na kilo zako sahihi ni zipi, kwani uzito anaopaswa kuwa nao mtu unategemea urefu wake.

Kwa mfano, kama urefu wako ni futi 5.7, uzito wako unaokubalika kiafya ni kati ya kilo 55 na 70, ukizidi hapo, hasa kuanzia kilo 80 hadi 100, uko katika hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa ya moyo na magonjwa mengine ya viungo, hivyo huna budi kuchukua hatua za haraka za kupunguza uzito.

Kitu kingine muhimu cha kuelewa ni kwamba unaweza kuwa na uzito unaokubalika kiafya, lakini ukawa huli matunda, mbogamboga na nafaka halisi hivyo ukawa una upungufu wa virutubisho muhimu mwilini. Kuwa na mwili mchangamfu na wenye afya njema ndiyo kitu muhimu zaidi, bila kujali una uzito gani.

Kwa wale wanaofanya mazoezi makali, kama vile kunyanyua vyuma, kucheza karate, n.k, jedwali letu linaweza kuwa siyo kipimo sahihi sana cha uzito wao. Wanashauriwa kupima upana wa kiuno. Wanaume wenye kiuno zaidi ya nchi 40 na wanawake wenye kiuno zaidi ya nchi 35, wako kwenye hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na magonjwa mengine ya moyo.

Ukitaka kupima kiuno chako, chukua tepu ya nguo (measure tape), vua shati ama blauzi kisha jipime eneo la chini ya tumbo kama unavyopimwa na fundi nguo saizi ya kiuno. Bila kubana mwili wako, shusha pumzi, tulia kisha jipime.

Sasa umefika wakati wa kupunguza uzito na unahitaji kujua utapunguza vipi na kitu gani kinatumika kama kichochoe katika suala zima la uzito wako. Kama nilivyowahi kudokeza katika makala zangu zilizopita, kiwango cha kalori (calories) anachokula mtu, ndicho ambacho kinachotawala uzito wa mtu. Unaweza kuuliza kalori nini?

Kwa kifupi, kalori ni njia ya kisayansi inayotumika kupima nishati ya mwili. Unahitaji kukisia kwa siku unaingiza mwilini kalori ngapi na unahitaji kiasi gani cha kalori kutokana na shughuli unazozifanya. Kwa sababu shughuli unazozifanya kila siku na chakula unachokula vinategemeana wakati wa kupunguza uzito. Kwa wastani mtu mzima kwa siku anahitaji kalori 2500 – 3000.

Kwa ujumla mazoezi au kujishughulisha kila siku ni muhimu kiafya. Mazoezi huusaidia mwili kufanya kazi yake vizuri na kudhibiti uzito kwa kuchoma kalori unazoingiza mwilini kama chakula na vinywaji kila siku.

FOMULA YA KUIMARISHA UZITO
Iili ubaki na uzito ulionao, kiwango cha kalori (chakula na vinywaji unavyokunywa) lazima kilingane na kalori unazozitoa (kwa njia ya kutumika mwilini, kwa njia ya mazoezi au kazi unazozifanya).

FOMULA YA KUPUNGUZA UZITO
Ili upunguze uzito, kiasi cha kalori unachokula lazima kiwe kidogo kuliko kile kinachotoka. Kwa maneno mengine, ule kidogo, ufanyekazi au mazoezi sana.

FOMULA YA KUONGEZA UZITO
Ili uongeze uzito, basi huna budi kula kiasi kikubwa cha kalori na utoe kiasi kidogo au kwa maneno mengine, ule sana ufanyekazi kidogo. Somo letu la leo ni kupunguza uzito, hivyo tutazungumzia hilo tu.

Kuchukua hatua ya mwanzo ya kuanza programu ya kupunguza uzito, unatakiwa ujiulize aina ya kazi unazozifanya kila siku; zikoje? Unahitaji kujiuliza kazi zako ili ujue kiwango cha kalori (chakula) unachohitaji kwa siku. Kazi zimegawanywa katika makundi matatu ambayo ni kazi nyepesi, kazi za wastani na kazi ngumu.

Hapa tuna maana kiwango cha shughuli zako za kila siku ambazo zinatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mtu anayefanyakazi za kubeba mizigo mahitaji ya kalori (chakula) yanatofautiana na mtu anayefanyakazi ofisini.

Itaendelea wiki ijayo..