KAMA UNABEEP WEWE KENGE TUKwa kifupi naweza kusema sasa mzuka umempanda tena, kama ilivyokuwa jina la lebo yao (Mzuka Records) au kitambo kile wakati anatoka na ngoma kama Mwanangu huna nidhamu, Kunguru hafugiki, Nakupenda tu na nyingine ambazo zilimfanya aonekane ana njaa ya kuwa juu.
Mchizi anaitwa Godfrey Tumaini a.k.a Ze Dudu, Baba Willy na mwaka huu wa 2009 anajiita Mamba, ili kudhihirisha hilo hivi juzi tu ameachia pini mpya yenye jina hilo (Mamba) akiwa na wale mapacha waliowahi kupiga shoo za kusisimua kwenye shindano la Bongo Star Search 2006 ambao wamekamata vesi ya pili.
ShowBiz ilipata bahati ya kuisikiliza ngoma hiyo ndani ya studio za Mzuka Records zilizopo Bahari Beach, Dar es Salaam kabla hata haijaanza kwenda hewani na kugundua kwamba, mzuka wa ‘Ze Dudu’ hivi sasa umepanda zaidi kana kwamba ndiyo anataka kutoka.
Akisema na safu hii, mchizi alitamka kwamba, ngoma hiyo inamtambulisha yeye kama ‘Mamba’ na wale wote ambao hawajiwezi kwa mambo mengi anawaita Kenge. “Kama unateta wenzio we kenge, kama una ‘beep’ we ni kenge, kama hununui bia we ni kenge, kama hauvai we ni kenge,”.
Aidha, Dudu alisema kwamba, hiyo yote ni sanaa tu, kama kuna mtu atahisi hiyo ngoma imemlenga yeye ni juu yake. Kiukweli ni bonge moja la Hip Hop ambalo litamrudisha msanii huyo juu kama alivyokuwa zamani. Siku zote sisi ShowBiz huwa hatuongea sana, icheki ngoma yenyewe hapo kushoto.
*****************************

HADIJA SURE NJE
Htimaye shindano la kumtafuta staa wa kike mwenye mvuto wa kimapenzi, ‘Ijumaa Sexiest Girl’ limebaki na washiriki wawili, Wema Sepetu na Irene Uwoya baada ya Hadija Sure kuambulia kura chache kutoka kwa majaji ambao ni wasomaji na hatimaye kutoka leo.
Mratibu wa shindano hili, Oscar Ndauka amesema kuwa, sasa wasomaji na wapenzi wa mpambano huu wanatakiwa wamtaje mshindi mmoja kati ya hawa wawili waliyobaki kabla ya kumtangaza mshindi siku kadhaa zijazo.
“Bado utaratibu wa kumtafuta mshindi uko vile vile, unachotakiwa kufanya kuandika ujumbe mfupi (SMS) ukimtaja mshiriki ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi, kisha tuma kwenda simu namba 0784-275 714,” alisema Ndauka.

No comments:
Post a Comment