Friday, February 6, 2009

BUSHOKE na mastaa kibao kuanza kazi Mwanza kesho

Mkurugenzi wa Zizzou Entertaiment, Tippo Athuman akiongea na press jana kuhusu ziara ya uzinduzi wa albamu ya Bushoke (kulia) jijini Mwanza.
Bushoke, akiongea na Press jana kuhusu tour yake ya Mwanza
Dogo Mfaume (kushoto), Blue na Maunda (kulia) wakiwa katika press jana
Baadhi ya wasanii watakaofanya makamuzi ya nguvu Mwanza

Ngwea (kulia) akiwa na msanii mwenzake wakitoka kwenye Press Conference

Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Kanda ya Ziwa, hasa wapenzi wa burudani imewadia, kesho Jumamosi ndani ya ukumbi wa Yatch Club, msanii Rutta Maximilian Bushoke akiwa na timu ya mastaa kibao wa Bongo Flava wataangusha shoo ya kutosha kwa ajili ya utambulisho wa albamu yake, ‘Dunia njia’, Amina Salim anashuka nayo.

Siku chache kabla hajadondoka jijini Mwanza, Bushoke alipiga stori na ShowBiz na kutamka kwamba, uzinduzi huo utageuka bonge la tamasha kwa kuwa utapambwa na mastaa wengi kama Mr. Blue, Ngwea, Squeezer na Steve kutoka Zizzou Entertainment, bila kuwasahau Chid Benz na Dogo Mfaume.

“Baada ya Yatch Club, Jumamosi (kesho), Jumapili tutaendelea na utambulisho wa albamu hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwa kiingilio cha shilingi 2000 kwa kila mtu. Tukitoka Mwanza msafara utaelekea Mkoani Mbeya ambapo shoo zitagongwa katika sehemu zitakazotajwa hivi karibuni, mashabiki wa huko wajiandae,” alisema Bushoke.

Albamu hii, ‘Dunia Njia’ ambayo ni ya tatu kwa Bushoke ina tofauti kubwa na nyingine zilizotangulia, kwanza imesheheni ngoma zaidi ya kumi, pili kazi zote zilizomo ndani yake zitamfanya msikilizaji asijutie kuinunua, yaani mchizi kafanya kila aina ya muziki, huku akiwa amevishirikisha vichwa kibao. Kwa kifupi jamaa kafanya kazi ya nguvu.
compiled by mc george

No comments: