Thursday, February 5, 2009

BUSHOKE YU TAYARI!

Mkurugenzi wa Zizzou Entertainment, Tippo Athuman (kati) akitabasamu wakati akiongea katika Press Conference leo kuhusu uzinduzi wa albamu ya Bushoke ' Dunia Njia' itakayofanyika jijni Mwanza Jumamosi ijayo.
Wasanii, Ngwea (kulia) na Bushoke wakimsikiliza bosi wao wakati akiongea na Media mchana leo.
Kijana anayesumbua kwa sana kwenye medani ya muziki wa Mchiriku, Dogo Mfaume, ambaye kwa sasa anatamba na 'pini' yake ya 'Kazi ya Dukani', naye atakuwepo kwenye uzinduzi wa Dunia Njia jijini Mwanza.
Ngwea na Steve (kulia) mara baada ya kuongea na media walipata wasaa wa kupozi kwa ajili ya picha, nje ya ofisi za Zizzou Fashions zilizopo maeneo ya Victoria, Kijitonyama jijini Dar es salaam.

1 comment:

Anonymous said...

Ngwea pole naona una bandage mkononi,vipi ulipata ajali?Pole sana kwa maumivu