Monday, September 28, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Raveen Tandon atoa uroda kwa mmoja tu!
Maombi kutoka kwa wasomaji wengi wa ‘Ebwana dah!’ akiwemo Serafina wa Ifakara, Morogoro ni kutaka kufahamu staa wa Bollywood, Raveena Tandon amewahi kujiachia na wanaume wangapi. Ishu ni kwamba Tandon ametia fora katika safu hii baada ya kubainika kuwa amewahi kutoa penzi lake kwa staa mmoja tu wa kiume.

Kwa mujibu wa mtandao unaodili na issues za nani kaparamia kwa nani, Raveena ametoa uroda kwa mchizi, Anil Thadani ambaye yupo naye tangu mwaka 2004 kama mume. Kabla ya Anil na hata baada ya kutoka naye, Raveena hajawahi kuhusishwa na mtu mwingine yeyote, staa au raia mwema wa kawaida. Alizaliwa Oktoba 26, 1970 Mumbai, India, ana umri wa miaka 38 a.k.a zake ni Ravs na Mast Mast girl. Urefu wake ni futi 5.5. Macho yake ni meusi na nywele zake ni nyeusi, nyota yake ni Nge, dini yake ni Hindu na ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Bombay’s Meethibai.
******************

Afande Sele Vs Fella Bifu lao nani mkorofi?
Mgogoro unaochukua nafasi pana kwa sasa katika kiwanda cha Bongo Flava ni kuhusiana na Mfalme wa Rhymes anayeendelea kudumu, Suleiman Msindi a.k.a Afande Sele na Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’. Ishu iko hivi, Abby Cool & MC George over the weekend ilifanya interview na mastaa hao ambapo wa kwanza alikuwa Sele aliyesema kuwa Mkubwa amekuwa akimfanyia kitu kibaya kwa kutaka kumpoteza kwenye game.

“Fella hanipendi, nikifanya shoo na Wanaume mara nyingi ananizimia MIC au anakorofisha mitambo ili sauti yangu isisikike vizuri. Fella hanipendi na mimi najua hilo,” alisema Sele.

Akijibu hoja, Mkubwa alisema kuwa anasikitishwa na kauli za Afande na kwamba hakuna ukweli katika hilo na kuongeza kwamba ingekuwa vema mfalme huyo anayetokea pande za Moro akataja shoo ambazo alimzimia vyombo.

“Mimi naangalia mafanikio na maendeleo ya wasanii wa kundi langu, si kuendekeza roho mbaya kwa wengine,” alisema Mkubwa. Bifu ni hilo, nani mkorofi? Kama una data zimwage kupitia namba 0715-110 173 na 0713-355 517.
************************

Eliza

Eliza gupta apagawishwa na Kanumba BBA

The cutie-baby wa Kibongo ndani ya mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta amepagawa kunyetishwa kuwa kabla yeye hajaingia ndani ya nyumba, staa wa muvi, Steven Kanumba ‘The Greatest’ alikuwa mjengoni.

Eliza alidata kimtindo alipokuwa akiongea hili na lile wiki iliyopita na washiriki wa kiume BBA ambao walimweleza kuwa walipoingia siku ya kwanza, walikuwa na Kanumba. “Don’t tell me, Kanumba was here?” Eliza aliuliza kwa mshangao, hivyo kuonesha kuwa kumbe wakati The Greatest alipokuwa mjengoni na mastaa wengine wa Afrika, washiriki wa kike walikuwa hawajui kabisa kilichokuwa kikiendelea mjengoni.

… ndani ya bifu na Hannington

The Most Beautiful girl ndani ya mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta yupo ndani ya bifu na mshiriki kutoka Uganda, Hannington.

Eliza ambaye ndiye Head of House kwa wiki hii, amechukizwa na Hanningtona kutokana na Mganda huyo kumsemea maneno yasiyopendeza. Katika hilo, wiki iliyopita Eliza alitangaza kutumia mamlaka yake kama Mkuu wa Mjengo kwa kumtaja Hannington ili apigiwe kura ya kutoka na Waafrika waamue. Kutokana na hali hiyo, washiriki mbalimbali wamekuwa wakimtaka Hannington kumuomba msamaha Eliza lakini Mganda huyo alikuwa mgumu kabla ya wikiendi iliyopita kutangaza kufanya hivyo mara Mtanzania huyo atakapotuliza hasira.
************

Mo Q
Ngwea

Ngwea kusimama na Mo Q
The Multi-Flavor on Bongo Flavor industry, Albert Mangwea ‘Ngwea’ yupo tayari kusimama na Mohamed Chalamila ‘Moe Q’ katika uzinduzi wa albamu ya ‘bwa mdogo’ huyo. Moe Q ataitambulisha albamu yake yenye jina la Machozi kwenye Ukumbi wa Travertine, Magomeni Oktoba 4, 2009 ambapo mbali na Ngwea, atapigwa tafu na Kundi la Jahazi Modern Taarab na wasanii wengine kibao.
***********

compiled by mc george

No comments: