Friday, October 2, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Shaa, D’banj, A.Y, Jay Kuangusha shoo kesho
MTV Africa Music Awards are now on peak na hapa tunadondosha news kwamba mchizi anayefanya vizuri kutoka pande wanapotokea P Square, Nigeria, Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a D’Banj atadondoka Bongo na kuangusha bonge la shoo kesho Jumamosi.

Inanyetishwa kuwa D’Banj atakuwa mgeni mwalikwa katika shoo iliyopewa jina la Road to MTV Africa Music Awards (MAMA), itakayochukua nafasi kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Oktoba 3, 2009.

Kwa mujibu wa mratibu wa ishu hiyo, Christina Mosha ‘Seven’ shoo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka katika sehemu tofauti, ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kunako tuzo hizo, safari hii itafanyika Bongo ambapo wakali wa Kibongo wanaowania tuzo hizo, Ambwene Yesaya ‘AY’ na Sara Kaisi ‘Shaa’ wataangusha burudani ya ukweli.

“Profesa Jay atakuwa mgeni mwalikwa katika tuzo hizo naye tutakuwa naye katika shoo hiyo ya Bilicanas ambayo itaanza saa tatu usiku na kuendelea kwa kiingilio cha shilingi 15, 000 kila mtu mmoja,” alisema Seven na kuongeza:

“Kwa maelezo zaidi Watanzania wanaweza kutembelea website yetu ambayo ni www.mama.mtvbase.com “Kumpigia kura A.Y andika neno BHH AY kisha unatuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333,” alisema.

50 Cent, Fat Joe ndani ya bifu kali
The Tuff Wallet MC’z, Fat Joe na 50 Cent wameendelea kunogesha uhasama baina yao na sasa ni kama vile bifu lao limenyunyiziwa petroli. Awali, 50 alianza shari kwa kuwadisi Fat na Jah Rule kabla ya mabepari hao on Hip Hop industry, kumgonga nyundo mchizi huyo wa G Unit katika wimbo ‘Am From New York’.

Kali iliyo gumzo ni kauli ya 50 kwamba aliugua ghafla na kuzidiwa kabla ya kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mount Sinai, Marekani baada ya kusikiliza pini zilizomo kwenye albamu mpya ya Fat Joe, ‘Jealous One Still an Envy’ nakala ya pili (J.O.S.E II ).

Hata hivyo, 50 alijieleza kuwa kilichomfanya azidiwe ni jinsi nyimbo za Fat Joe zilivyo na kiwango kibovu na kwamba zilimuumiza masikio. Baada ya kauli hiyo, Fat Joe kupitia ukurasa wake wa Twitter alimjibu 50 akae mbali naye na kama kachanganyikiwa kwa pini zake na kuongeza kwamba nyimbo zilizomo kwenye JOSE II ndiyo kiwango cha wanamuziki wa ukweli.
****************************************

Mo Q yupo tayari kwa J’2
Mchizi anayesimama ngangari kwenye game la Bongo Flava, Mohamed Chalamila ‘Moe Q’ yupo tayari kwa ajili ya uzinduzi wa albamu yake inayoitwa Machozi, kwenye Ukumbi wa Travertine, Magomeni, Dar.

Moe Q ambaye ni mdogo wa staa wa Bongo Flava, Rehema Chalamila ‘Ray C’ anatarajiwa kupigwa tafu na wakali, Albert Mangwea ‘Ngwair’, Jahazi Modern Taarab na wengineo.
*****************************************

Fella kugonga Video ya Mkubwa na wanawe
Mshikadau mwenye uzani mkubwa on Bongo Flava, Said Fella ‘Mkubwa’ yupo sawa kwa ajili ya video mpya ya wimbo Mkubwa na Wanawe ambayo amewashirikisha wana wa TMK Family.

“Kazi ya kugonga video hiyo imeanza jana, naamini ikikamilika itakuwa katika levo nyingine,” alisema.
*******************************************

Kalapina kumtoa Mau wa Kikosi
The First Lady wa Kikosi cha Mizinga yupo njiani kutoka na muda si mrefu ujao atakuwa hewani hewani na albamu yake mpya.

RaiS wa Kikosi, Karama Masoud ‘Kalapina’ alisema na safu hii kuwa ameamua kumtoa Mau ili kuonesha kuwa Bongo bado kuna wanawake wenye uwezo mkubwa wa kufanya Hip Hop.
****************************
COMPILED BY MC GEORGE

No comments: