Sunday, October 11, 2009

PRE-PARTY NA AFTER PARTY YA MTV_ NRB


..Kila kitu kikiwa tayari kwa kujirusha ndani ya Blue Times Club wakati wa Pre-Party ya MTV Music Awards with Zain zilizofikia tamati jana jijini Nairobi, ndani ya ukumbi wa michezo wa kimataifa wa Moi.
Troop kali la Codered DJs; kushoto ni DJ Star na kulia ni DJ George wakiendesha mashambulizi ya After Party ndani ya Blue Times, ukumbi uliyopo jirani na Club Afrique & Galileo, ilikuwa ni na maalum kwa washindi na washindwa wa tuzo za MAMA with Zain kujiachia.
Baada ya kuachia 'mziki mnene' wakati wa utoaji tuzo, Akon anapata nafasi ya kujiachia na shabiki ndani ya Blue Times
'Mchizi' Wyclef Jean naye kama kawaida yake alijichanganya kwenye After Party utafikiri siye yule aliyekuwa kule T na kamashani alikoteka shoo nzima kwa shoo kali...

Mshikaji wangu Henry Ssali wa gazeti la The Monitor la Uganda akijiachia na mwanadada Sabie kutoka Mnet South Africa
Mwakilishi wa MTV Africa-Tanzania Christine Mosha 'Seven' akila pozi na shoga'ke Clare ndani ya Blue Times
VJ machachari wa MTV wanakupa 'halla'! Kushoto ni Vj V wa TZ na Vj Fix wa Kenya, ndani ya After-Party

MTV Awards ilikuwa ni nafasi pia ya kukutana na marafiki wapya katika industry ya habari kutoka sehemu mbalimbali. Kutoka kushoto ni rafiki yangu Sammy Farson mtangazaji kutoka Citi FM ya Ghana, mwanadada Ndebele ambaye ni mwandishi wa Daily na Sunday Times la South Africa na Henry Ssali- Naibu Mhariri wa gazeti la The Monitor la Uganda
Marafiki zaidi, kutoka kulia: Ben wa Power FM Uganda, Simone wa Hype Magazine la South Africa, Tabie wa Mnet na Brian wa Multi Choice South Africa..nyama choma tamu!!!
Mmoja wa waandaji wa tamasha la MAMA, Belinda (kulia) wa MTV America akila shavu na mwandishi Ndebele wa Sunday Times ya South.
...cheers guys!!!!

No comments: