Tuesday, November 3, 2009

MATATIZO YA KIBOFU YANAWEZA KUTIBIKA KWA CHAKULA!


Matatizo ya kiafya katika kibofu cha mkojo yamekuwa mengi hivi sasa, hasa kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 50. Kazi kubwa ya kibofu ni kusaidia ukuaji wa mbegu za kiume, kama kibofu kikiwa na matatizo, uzalishaji wa mbegu za kiume nao hupungua sana na tatizo lisipotibiwa haraka, husababisha ugumba. Aina nyingine ya matatizo ya kibofu husababisha uvimbe sehemu za siri.Inaelezwa kuwa matatizo ya kibofu mara nyingi huwa ni ya kurithi, ingawa kuna sababu nyingine pia.

Ugonjwa unaweza kusambaa ukoo mzima, kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Sababu nyingine zinazosababisha ugonjwa huu zinaelezwa kuwa ni kukaa kwa muda mrefu, kuvaa nguo zinazobana, ukosefu wa choo na maambukizi. Kupenda kujamiina sana nako kunaelezwa kuwa ni sababu moja wapo. Pamoja na ukubwa wa tatizo hili ambalo husababisha kansa pia, kuna habari njema kuwa matatizo madogo ya kibofu yanaweza kutibiwa nyumbani kwa kula vyakula na kufuata kanuna kadhaa na mtu akapona kabisa au akazuia isimpate, lakini iwapo tatizo limeshakomaa na kuwa sugu, unashauriwa kwenda hospitali na kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.

UTAJUAJE UNA TATIZO?
Dalili moja wapo ya mtu mwenye tatizo la kibofu ni kusikia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo. Dalili nyingine ni kushindwa kukojoa kabisa licha ya kuhisi kubanwa na mkojo. Dalili nyingine ni kusikia maumivu chini ya mgongo na kwenye ‘hips’. Kwa kuwa mtu huwezi kujipima kama una tatizo hilo, ina shauriwa kwenda hispitali kupima. Saratani ya kibofu ni miongoni mwa matatizo yanayoweza kujitokeza na inaweza kuuawa!

DONDOO ZA TIBA MBADALA..
Tiba mbadala ya matatizo ya kibofu hufanyakazi vizuri na imeonesha mafanikio makubwa kwa watu waliowahi kujaribu. Mbegu za maboga ni miongoni mwa tiba mbadala za kutibu matatizo ya kibofu. Pondaponda kiasi cha mbegu 15 hadi 20 za maboga na changanya kwenye mlo wako wa kila siku.Utaona mabadiliko ya haraka ya unafuu ndani ya wiki mbili hadi tatu. Vitamini E ni kirutubisho muhimu sana katika kutibu matatizo ya kibofu. Aidha, mboga za majani rangi ya kijani, mayai na bidhaa zitokanazo na maziwa nazo zina kiwango kikubwa cha vitamin E, hivyo viliwe kila siku.Dawa nyingine mbadala ya matatizo ya kibofu ni enema ya maji ya uvugu.

Enema ya aina hii ifanywe mara mbili au tatu kwa wiki ili kurejesha utendaji wake wa kawaida. Uvutaji sigara na unywaji pombe hauruhusiwi kabisa wakati wa kufanya tiba hizi, hali kadhalika vyakula vilivyoungwa sana. Mwisho, inashauriwa sana kuacha kunywa vinywaji vyote vyenye ‘caffeine’, hii ni pamoja na chai na kahawa, kwa sababu huzalisha matizo zaidi. Mazoezi ya nusu saa ya kukimbia au kuendesha baiskeli yatasaidia zaidi. Kwa kuwa baridi ni miongoni mwa sababu zinazochangia maradhi ya kibofu, mgonjwa anayeishi sehemu yenye baridi anashauriwa kuhamia sehemu yenye joto.

No comments: