Monday, November 2, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!



Unga unaimeng’enya Bongo Flava
Mambo hayapo ok, Bongo Flava inazidi kumeng’enywa na nguvu kazi yake inapungua. Hapa ni gumzo kuwa vijana wengi wapo kwenye skendo ya kutumia dawa za kulevya.

Kuna maswali magumu; Kwanini baadhi ya wasanii wana-shine kidogo, wanakubalika kitaa na kiasi fulani maisha yao kuwa bora lakini ghafla tu madogo wanaonekana kitaa wamechoka na afya zimekuwa dhaifu.

Madai ya msingi ni matumizi ya dawa za kulevya a.k.a unga, kwamba madogo wengi wakishakubalika kitaa kwa njia moja au nyingine hujiingiza kwenye matumizi ya unga, wanabwia na wengine wanajidunga kabisa.

Its dangerous! The only gent on kundi marehemu la Wakilisha, Langa Kileo anaweza kuwa mfano hai, baada ya kukiri kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa iliyopita kuwa alikuwa anabwia unga lakini sasa amestop. Langa alisema kuwa alikuwa mbwiaji mzuri wa Cocktail kabla ya hivi karibuni kuugua typhoid, hivyo kukosa access ya kupata unga.

Alisema, alianza kama utani lakini baadaye alizidiwa na akawa hawezi kuacha, ingawa sasa hivi anamshukuru Mungu kwamba yamepita. Katika hilo, Langa alieleza kwamba angalau sasa anajisikia nafuu na afya imeanza kurejea. Hiyo ni kauli ya Langa kupitia session ya Crazy Friday, lakini ukweli ni kuwa madogo kibao wapo kwenye skendo ya kubwia.

Albert Mangwea ‘Ngwair’, Heri Samir ‘Blu’ Mark II B a.k.a Simba ni kati ya majina ambayo yanatajwa kwenye orodha ya wanaodaiwa kubwia unga. Hayo ni majina yanayotajwa lakini nyuma ya pazia ni wengi na hii inasababisha kizazi kipya kisiwe na afya standard. Madogo wanasimama vizuri lakini baadaye wanakuwa dhoofu l’hali. Hii ni hatari na sisi kama wadau tunalaani vikali matumizi ya dawa za kulevya.
**************************
BBA: Eliza aanza kuachia taratibu
Ukaribu wa Cutie Baby wa Bongo, Elizabeth Gupta ‘Queen’ na Mnigeria Kevin umeanza kuzua mambo na tayari alama ya hatari imekwishaanza kuonekana.

Tayari Eliza amekwishaliwa denda na Kevin, hivyo kuibua shaka kuwa one day anaweza kuachia ustaarabu wake wote, ingawa kwa mbali bado ni mgumu. Mbali na ishu hiyo ya denda, Alhamisi iliyopita, Eliza alikuwa ni full kujiachia mbele ya Kevin ambapo aliweza kumruhusu Kevin amnyonye chini ya mdomo, wakati yeye alimnyonya Mnigeria huyo mkononi.

Hata hivyo, katika zoezi hilo la kunyonyana sehemu mbalimbali, wapo waliofika mbali zaidi kwa kuruhusu sehemu zao za kiuno, macho na kadhalika.
****************

D’Banj awalisha washiriki chakula cha Nigeria
Staa aliye juu kwenye game barani Afrika kwa sasa, D’Banj a.k.a Kokomaster amewapa fleva tofauti ya maakuli, washiriki wote wa mjengo wa Big Brother Revolution kwa kuwapikia mapishi ya Kinigeria.

D’Banj aliwapikia washiriki chakula hicho, baada ya kualikwa kwenye jumba hilo na kujumuika na washiriki wengine ambapo mbali na kuwalisha mapishi ya Kinigeria, pia alitoa zawadi. Zawadi ambazo mwanamuziki huyo wa Nigeria alizitoa ni t-shirts kwa wasanii wote pamoja na miwani kwa wachache walioshinda shindano alilowaandalia.

Washiriki waliofanikiwa kunyakuwa miwani ni Nkenna, Itai na Kevin, wakati kwa jumla kila mtu alifurahia chakula kilichoandaliwa na staa huyo ambaye alionesha uwezo mkubwa wapo jukwaani.
**************


Eliza ana siri nzito moyoni
The Most Beautiful Girl ndani ya mjengo wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta ana siri nzito moyoni na alilidhihirisha hilo wikiendi iliyopita alipokuwa anazungumza na Kevin.

Eliza akiwa ameketi na Kevin, ghafla aliangua kilio na kumueleza brazameni huyo wa Nigeria kwamba kuna siri nzito ambayo inamtesa moyoni kwa muda mrefu. Mtizedi huyo alionesha mwanga wa kusimulia, aliposema kuwa siri yenyewe inamhusu yeye na mfanyabiashara mmoja lakini alishindwa kumalizia stori hiyo baada ya Emma kuvamia na kumkuta Eliza akiwa ana alama za machozi.

Emma alipotaka kujua Eliza analia nini, hakupata majibu sahihi kwani Kevin aliingilia kati na kujitaja yeye kwamba ndiye amemuudhi. Hata hivyo, Eliza hakuweza kuendelea na stori hiyo na hakuthubutu kumsimulia Kevin hata baada ya Emma kuondoka.
*************
Busta Rhymes Kufiestika Bongo kwa vocal za kigumu
Siyo stori kwamba Busta Rhymes atakuwa Bongo wikiendi hii na atapiga shoo kali kwenye Viwanja vya Posta, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Mikocheni, Dar es Salaam. Busta, staa wa Hip Hop mwenye vocal za kigumu, atawafiestisha Wabongo kwenye viwanja hivyo ambavyo vinatazamana na chuo cha ustawi wa jamii, Kijitonyama, jijini Dar.

Mchizi huyo wa Marekani, anatua Bongo kwa ajili ya kushoo love na wana wa himaya ya JK, wakati wa shoo kali ya Fiesta 2009 ambayo mwaka huu inatambaa na slogan inayonena ‘One Love’. Akiwa Bongo, Busta atashirikiana na wakali kibao wa Bongo ambao wapo kwenye chati na kusababisha kwa burudani ya daraja la next level.

Mbali na Fiesta, hapa Ebwana Dah inamtambalia ambapo katika listi iliyo wazi ni kwamba mchizi amewahi kutoka watoto wa jinsi ya kike watatu. Karrine Steffans ndiye anatajwa nambari wani kutoka na Busta, wakati Nicole Richie anaungwa, ingawa haitajwi ni lini alichangamka nao kimalavi davi. Mwaka 1998, mchizi alianza kuchizika on bed na Eden Harel na yupo naye mpaka nukta hii.

Jina lake kamili ni Trevor Tahiem Smith, Jr., umri wake ni miaka 37, alizaliwa Mei 20, 1972, Hempstead, New York, Marekani. Ng’ombe ndiyo nyota yake na ni msomi wa Uniondale High School.
********************************


Temba, Chegge Kusepa Dubai, Wahu naye...
Machizi wanaoifanya TMK Wanaume Family iwe on top kwa sasa, Amani James Temba ‘Mheshimiwa’ na Said Juma ‘Chegge’ wanatarajiwa kudondoka pande za Dubai na kufanya shoo ya ukweli.


Chegge na Mh. Temba watakuwa Dubai ambapo jukumu lao ni kutoa shoo zitakazofanyika Novemba 5 na 6, mwaka huu lakini Novemba 7 watakuwa Dar na kufanya vitu vikali na kuinogesha Fiesta 2009.

Temba alichonga na uwanja huu kuwa kila kitu kipo confirmed na kwamba tayari wameshaanza maandalizi ya kupiga shoo hiyo ambayo wamekwishavuta mzigo nusu. Mbali na hilo, kupitia hapa unaweza kupewa information kuwa video ya wimbo Running Low ya Wahu ambaye ni mtoto wa Kenya na Chegge a.k.a Mtoto wa Mama Said siku chache zijazo itakuwa kideoni.
**************************

Rose Muhando Kujirusha na Mhe. Mbunge!
Muimba Injili maarufu nchini, Rose Muhando anatarajiwa kuwakata kiu wakazi wa jijini Mwanza wakati atakapopanda jukwaani kutumbuiza katika tamasha la wazi kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba.

Katika tamasha hilo litakalofanyika Novemba 29, 2009, Rose Muhando atajirusha stejini sambamba na mbunge wa Viti Maalum kwa ‘leseni’ ya CCM, Mheshimiwa Martha Mlata ambaye pia ni msanii wa nyimbo za Injili, bila kumsahau Mzee Makassy ambaye pia atapanda jukwaani siku hiyo.

Kwa mujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Stella Joel, wanamuziki wengine watakaodandia stejini siku hiyo sambamba na Rose, Martha na Mzee Makassy ni John Shaaban, yeye mwenyewe huku akisisitiza kuwa, maandalizi yote yamekamilika.
**************************
compiled by mc george

No comments: