Saturday, October 31, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Enji

“Kina Ray C hawanisumbui kwenye game”
AKiwa anasimama na ngoma yake moja tu yenye jina la ‘Wewe’ aliyompa shavu Chid Benz, Msanii mrembo anayepitia ndani ya shindano la Bongo Star Search 2007, Angelis Faber a.k.a Enji amesema na Showbiz kwamba kutokana na uwezo alionao kwenye mradi huo, haamini kama yupo msanii wa kike anayeweza kumsumbua hasa atakapoamua kupiga game ‘siriasi’, Christopher Lissa anashuka na full data.

Enji alisema kuwa, wapo baadhi ya watu wanaodhani hataweza kusonga zaidi kimuziki hasa baada ya kutoa ngoma hiyo iliyofanyika kupitia Dhahabu Records. “Nina uwezo mkubwa wa kufanya muziki, kina Ray C hawanisumbui kwa sababu muziki kwangu ni kipaji, upo kwenye damu na pia ndiyo kila kitu kwangu ila kwasasa bado sijaamua kuelekeza mashambulizi huko,” alisema Enji.

Mwana Bongo Flava huyo ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kike wenye mvuto wa kimahaba, aliongeza kuwa hivi sasa hafanyi muziki kwa kuusotea sana ‘kuhaso’ kama walivyo ‘atisti’ wengine wa Kibongo kwakuwa yuko bize na masomo. “Muziki unahitaji muda na nafasi ya kutosha. Nitafanya wakati muafaka utakapofika, nikimaliza masomo,” alisema.
*******************************************

Temba: “Watu hawaamini kama nilibeba bunduki”
Kutoka ndani ya Kundi la TMK Wanaume family, msanii Amani James Temba a.k.a Mhe. Temba amesema na Showbiz kwamba, siku kadhaa baada ya gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda kuandika ishu ya yeye kubeba mtutu wa bunduki begani alipokuwa nchini Liberia hivi karibuni, baadhi ya watu wawakiwemo mashabiki wake bado hawajaamini kama ni kweli.

“Yaani ile picha ilipotoka gazetini tu, watu kibao wakiwemo washkaji zangu wa karibu hawajaamini, wanasema kwamba siwezi kubeba bunduki nikajiachia nayo kivile. Wengine wanasema kuwa picha imetegenezwa kwa kompyuta, mimi nawashangaa mbona nilishawahi kubeba mara kibao nilipokuwa jeshini?” Alihoji Temba.

Msanii huyo na kundi lake la TMK pamoja na Tip Top Connection leo wanatarajia kudondosha shoo ya ukweli pande za Geita, Mwanza, ikifuatiwa na Bukoba kesho Jumamosi, ndani ya Linas Klabu, kisha kunako Uwanja wa Kaitaba siku ya Jumapili.
**********************************

Rakim amchana Jigga
Mwana Hip Hop wa kitambo nchini Marekani, Rakim ameibuka na kumchana vibaya mkali wa miondoko hiyo, Jay- Z a.k.a Jigga.

Akipiga stori na mtandao wa Allhiphop hivi karibuni, Rakim alitoa maneno makali yaliyoonekana kumgonga Jay-Z moja kwa moja, huku akipinga kitendo cha rapa huyo kujiita mfalme wa Hip Hop.

“Nimechoshwa na upuuzi unaoenezwa na vijana hivi sasa kwenye game, wengine wanadiriki kujipa ufalme, wengine wanatangaza Hip Hop imekufa huu ni upuuzi. Hawakumbuki kama Hip Hop ilikuwepo hata kabla wao hawajazaliwa,” alisema Rakim.
******************************************
Chriss Brown amkumbuka Rihanna
Mwanamuziki Chris Brown ambaye hivi karibuni alihukumiwa kifungo cha kukaa mbali na aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna baada ya kupatikana na hatia ya kumdunda mrembo huyo alionekana kumkumbuka kwa kumuandikia ujumbe wa kumuomba msamaha.

Mbali na kumuandikia ujumbe mzuri wa kurudisha ukaribu wao, Brown pia aliweka baadhi ya vipande vya video mbalimbali kunako mtandao wa You Tube vilivyomuonesha yeye na Rihanna wakishea vitu kadhaa kabla ya ugomvi wao.

Mbali na kuhukumiwa kutomkaribia wala kumpigia simu Rihanna kwa muda wa miaka kadhaa, adhabu nyingine iliyomkumba Brown katika kesi hiyo ni pamoja na kifungo cha nje ambacho adhabu yake ni kufanya kazi za kijamii.
*************************************************


Madonna full kujiachia Afrika
Baada ya kumuasili mtoto David Banda wa Malawi miaka kadhaa iliyopita, mwanamuziki mkongwe, Madonna kutoka pande za Marekani ameonekana kuvutiwa zaidi na Afrika kwani hivi karibuni alidondoka tena pande hizo za Malawi na kufungua shule ya watoto wa kike.

Msanii huyo ambaye aliongozana na mtoto wake aliyemuasili nchi humo, alionekana mwenye furaha kwa kufanikiwa kufungua shule hiyo iliyopo kunako kijiji cha Chinkhota.

Mbali na Banda mtoto mwingine ambaye Madonna alifanikiwa kumuasili katika nchi hiyo ni Mercy James.
************************************

compiled: by mc george

1 comment:

Anonymous said...

Kweli mimi nampenda sana huyu dada madona kwa jinsi anavyoonyesha upendo alionao kwa watu walio pinda kimaisha,hongera sana madona.