Fainali Des. 20 TCC Club, Twanga Pepeta kufunika
Shindano la kumpata handsome boy mwenye jina kubwa nchini, Ijumaa Sexiest Bachelor, linaelekea ukiongoni na Desemba 20, 2009 ndiyo fainali yenyewe.
Fainali ya kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, itafanyika kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo mastaa wanne, waliobaki mmoja wao atakabidhiwa taji.
Shoo ya kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor mwaka huu, itasindikizwa na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambayo kwa sasa inatawala soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake zilizopo kwenye chati.
Handsome Boys, Hemed Suleiman, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Yusuf Mlela na Steven Kanumba, kati yao ataibuka na taji hilo linaloheshimiwa zaidi na wadau wa burudani nchini.
Steven Kanumba ndiye anayeshikilia taji hilo ambalo alilitwaa mwaka juzi baada ya kumwaga kwenye fainali, golikipa wa Simba, Juma Kaseja kwa kura chache na romantic vocalist wa Bongo Flava, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’ aliambulia nafasi ya tatu.
Ni nani anayedatisha, Hemed, Kanumba, Yusuf au Marlaw? Jibu litapatikana Jumapili ya Desemba 20, ndani ya TCC Club, huku burudani ya kutakata ‘ikifanzwa’ kwa ukamilifu na Twanga.
Hapa Saleh Kupaza, pale Kalala Junior, huku Chalz Baba, kati amesimama Khaleed Chokoraa, kionjo cha kike kinatoka kwa Luiza Mbutu, utamu unakolezwa na kisigino cha Ferguson, MCD ndani, Amigolas, Lillian Internet, Aisha Madinda. Itakuwa shoo ‘babkubwa’.
Endelea kumpigia kura mshiriki unayempenda kwa kuandika namba yake kisha tuma kwenda 15551.
The very strong sterling ndani ya Bongo Flava industry, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ yupo hewani kwa mara nyingine na sasa anakuja na mawe 10 yaliyosimama kama madini ya dhahabu ndani ya albamu yake ya 10 inayosimama kwa jina la Veto.
Mr. II a.k.a Sugu ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mzigo kamili umeandaliwa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo.
Stigo ‘amefanza’ mawe saba na Puzo amegonga mawili, huku wana-Hip Hop wenye heshima Bongland kama Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’ kwa pamoja wameingiza vocal kwenye albamu hiyo.
Wamarekani wawili, Andre ambaye ni mchizi pamoja na mwanadada Shanice, wameingiza sauti na kukamilisha ujio mpya wa Sugu ambaye tangu mwaka 1994, kila akitoka mandhari ya Bongo hubadilika kutokana na vishindo vyake.
Moto wa Diamond Mkesha wa Krismasi, utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 (15th Anniversary) ya Sugu ndani ya game ya Bongo Flava, kwani tangu mwaka 1994, bado ametuama pale pale on top.
Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava, kijana Ambwene Yesaya ametoka tena, safari hii kasimama wima na mrembo Jokate Mwegelo kunako Kings and Queens yakiwa ni mapinduzi mengine kunako sanaa yake, pia ni maandalizi ya kuufunga mwaka 2009 na kuufungua 2010.
Akipiga stori na ShowBiz muda mchache baada ya kudondoka Bongo akitokea pande za Kenya, alikokwenda kukmilisha michongo hiyo mchizi alisema kwamba ngoma ya Kings and Queens itatoka kwa staili ya video na kwamba kabla ya kusambaa kwenye runinga za TZ itaanza kuonekana MTV.
“Mbali na video hiyo ambayo nimeigonga Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa pia kwa upande wa redio nimeachia kazi nyingine yenye jina la Bed and Breakfast ambayo imeifanyika ndani ya studio za B. Hitz Music Group chini ya Prodyuza Hermy B,” alisema A.Y.
Kitu kingine kipya alichosema Ambwene ni kwamba, kazi hiyo imefanyiwa mautundu zaidi (Mastering) katika studio za Ogopa Deejays. “Siku chache zijazo natarajia kwenda kupiga video yake na Kampuni ya Film Online iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini. Nawashukuru sana fans wangu, msichoke kunisapogti, sitawaangusha,” alisema.
compiled by mc george
Shindano la kumpata handsome boy mwenye jina kubwa nchini, Ijumaa Sexiest Bachelor, linaelekea ukiongoni na Desemba 20, 2009 ndiyo fainali yenyewe.
Fainali ya kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, itafanyika kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe, jijini Dar es Salaam ambapo mastaa wanne, waliobaki mmoja wao atakabidhiwa taji.
Shoo ya kumpata Ijumaa Sexiest Bachelor mwaka huu, itasindikizwa na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ ambayo kwa sasa inatawala soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake zilizopo kwenye chati.
Handsome Boys, Hemed Suleiman, Lawrence Malima ‘Marlaw’, Yusuf Mlela na Steven Kanumba, kati yao ataibuka na taji hilo linaloheshimiwa zaidi na wadau wa burudani nchini.
Steven Kanumba ndiye anayeshikilia taji hilo ambalo alilitwaa mwaka juzi baada ya kumwaga kwenye fainali, golikipa wa Simba, Juma Kaseja kwa kura chache na romantic vocalist wa Bongo Flava, Aboubakar Katwila ‘Q Chillah’ aliambulia nafasi ya tatu.
Ni nani anayedatisha, Hemed, Kanumba, Yusuf au Marlaw? Jibu litapatikana Jumapili ya Desemba 20, ndani ya TCC Club, huku burudani ya kutakata ‘ikifanzwa’ kwa ukamilifu na Twanga.
Hapa Saleh Kupaza, pale Kalala Junior, huku Chalz Baba, kati amesimama Khaleed Chokoraa, kionjo cha kike kinatoka kwa Luiza Mbutu, utamu unakolezwa na kisigino cha Ferguson, MCD ndani, Amigolas, Lillian Internet, Aisha Madinda. Itakuwa shoo ‘babkubwa’.
Endelea kumpigia kura mshiriki unayempenda kwa kuandika namba yake kisha tuma kwenda 15551.
********************************************************
Sugu: Katika Veto na mawe 10 ya dhahabuThe very strong sterling ndani ya Bongo Flava industry, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ yupo hewani kwa mara nyingine na sasa anakuja na mawe 10 yaliyosimama kama madini ya dhahabu ndani ya albamu yake ya 10 inayosimama kwa jina la Veto.
Mr. II a.k.a Sugu ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Mzigo kamili umeandaliwa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo.
Stigo ‘amefanza’ mawe saba na Puzo amegonga mawili, huku wana-Hip Hop wenye heshima Bongland kama Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’ kwa pamoja wameingiza vocal kwenye albamu hiyo.
Wamarekani wawili, Andre ambaye ni mchizi pamoja na mwanadada Shanice, wameingiza sauti na kukamilisha ujio mpya wa Sugu ambaye tangu mwaka 1994, kila akitoka mandhari ya Bongo hubadilika kutokana na vishindo vyake.
Moto wa Diamond Mkesha wa Krismasi, utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 (15th Anniversary) ya Sugu ndani ya game ya Bongo Flava, kwani tangu mwaka 1994, bado ametuama pale pale on top.
********************************************
Wagonga Kings and QueensKutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Flava, kijana Ambwene Yesaya ametoka tena, safari hii kasimama wima na mrembo Jokate Mwegelo kunako Kings and Queens yakiwa ni mapinduzi mengine kunako sanaa yake, pia ni maandalizi ya kuufunga mwaka 2009 na kuufungua 2010.
Akipiga stori na ShowBiz muda mchache baada ya kudondoka Bongo akitokea pande za Kenya, alikokwenda kukmilisha michongo hiyo mchizi alisema kwamba ngoma ya Kings and Queens itatoka kwa staili ya video na kwamba kabla ya kusambaa kwenye runinga za TZ itaanza kuonekana MTV.
“Mbali na video hiyo ambayo nimeigonga Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa pia kwa upande wa redio nimeachia kazi nyingine yenye jina la Bed and Breakfast ambayo imeifanyika ndani ya studio za B. Hitz Music Group chini ya Prodyuza Hermy B,” alisema A.Y.
Kitu kingine kipya alichosema Ambwene ni kwamba, kazi hiyo imefanyiwa mautundu zaidi (Mastering) katika studio za Ogopa Deejays. “Siku chache zijazo natarajia kwenda kupiga video yake na Kampuni ya Film Online iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini. Nawashukuru sana fans wangu, msichoke kunisapogti, sitawaangusha,” alisema.
compiled by mc george
No comments:
Post a Comment