Monday, December 14, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

********************************************
Sugu aja na mtikisiko Mkesha wa Krismasi
Mwana-Hip Hop mwenye mafanikio zaidi Bongo, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ au Sugu anarudi kamili na sasa yupo chimbo akijiandaa kwa ajili ya kufanya mtikisiko wa kihistoria, atakapokuwa anaitambulisha albamu yake ya 10 inayosimama kwa jina la Veto.

Mr. II a.k.a Sugu ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Mzigo kamili umeandaliwa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo, huku wakali wa Kibongo waliouza sauti ndani ya albamu hiyo wakiwa ni Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’.

Wamarekani wawili, Andre ambaye ni mchizi pamoja na mwanadada Shanice, wameingiza sauti na kukamilisha ujio mpya wa Sugu ambaye tangu mwaka 1994, kila akitoka mandhari ya Bongo hubadilika kutokana na vishindo vyake.

Katika kurekodi albamu hiyo, Balozi a.k.a Dolla Soul yupo kiwanja, hivyo ilikuwa rahisi kwake kuingiza vocal, FA alitembelea maskani ya Sugu, New York, kwahivyo alipotia maguu tu, akapelekwa studio kupayuka mtamboni.

Kwa upande wa Jizze na Johmakini, wao waliingiza vocal MJ Records kwa prodyuza Marco Challi na kuzituma kiwanja ambako alizikabidhi S&S Records, wakati Solo yeye alituma sauti akiwa nchini Ireland ambako anafanya maisha hivi sasa.

Moto wa Diamond Mkesha wa Krismasi, utaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 (15th Anniversary) ya Sugu ndani ya game ya Bongo Flava, kwani tangu mwaka 1994 bado ametuama pale pale on top.

Wakali wote wanaovuma kwa sasa wanatarajiwa kumpiga tafu Sugu ili kutoa shoo ya mapinduzi ya Bongo Flava. Mchizi alianza kurekodi mwaka 1994, singo ya kwanza ikapewa jina Siku Yangu, albamu ya kwanza ikaitwa Ni Mimi, zikaja Ndani ya Bongo, Niite Mr. II, Nje ya Bongo, Millennium, Muziki na Maisha, Itikadi, Sugu, Ujio wa Umri na sasa ni Veto.
*********************
Ebwana Dah!
Faith Evans: Hii ndiyo listi ya wanaume wake, pia usagaji
Mwanamke mwenye uwezo mkubwa kifedha, Faith Evans anaingia kwenye mjengo wa Ebwana Dah! Hapa inawekwa orodha ya wanaume wanaojulikana ambao kwa nyakati tofauti amekwea nao on bed.

Mtandao wa kiwanja unaodili na issuez za mastaa katika eneo la nani katoka na nani, unamuingiza Faith katika skendo ya usagaji kwamba amewahi kufanya ngono ya jinsia moja na staa mwenzake, Missy Elliot.

Imewekwa kweupe kuwa Faith na Missy walianza kukukuruka pamoja mwaka 1999 na haielezwi kama bado wanaendelea au waliachana.

Kwa upande wa wanaume, anayetajwa wa kwanza ni aliyekuwa mume wake, Christopher Wallace ‘Notorious B.I.G’, kwamba walikuwa pamoja kuanzia mwaka 1994 hadi 1997, wakati staa huyo wa Hip Hop alipouawa kwa risasi.

Rapa mwenye kismati, the heavy weight vocal, Tupac Shakur naye anatajwa kwenye listi kwamba mwaka 1995, alianguka kitandani na Faith, tukio ambalo linatajwa kuwa kiini cha yeye kuuawa mwaka 1996.

Pamoja na ushahidi kuwa butu mahakamani, lakini bado inadaiwa kuwa Tupac aliuawa ikiwa ni kisasi cha B.I.G na wapambe wake, baada ya staa huyo wa Hip Hop kutoka na mai waifu wake, Faith.

Todd Russaw naye anatajwa kwamba walianza kucharukiana mwaka 1998, wakati P. Diddy anachukua nafasi kutokana na maelezo kuwa kwa nyakati tofauti aliwahi kujirusha naye baada ya swahibu wake B.I.G kufariki.

P. Diddy hatajwi kwenye list ya Faith, lakini kwenye orodha ya wanawake waliowahi kutoka na P. Diddy, Faith yumo ndani.

Jina lake kamili ni Faith Renée Evans, umri wake ni miaka 36, alizaliwa June 10, 1973, Lakeland, Florida, Marekani. Hivi sasa ndiye anayemiliki zaidi ya 60% ya hisa za Kampuni ya Bad Boys Entertainment ambayo P. Diddy ndiye bosi wake.
compiled by mc george

1 comment:

Anonymous said...

....just kuelimishana,swala la usagaji na ushoga kwa wenzetu huku si skendo,ni maisha ya kila siku na ndo maana unasikia watu mashoga wanaoana siku hizi,kama ilivyo kwa TV presenter maarufu Ellen Degeneres ambaye ni msagaji na wengine wengi tu...