Monday, December 21, 2009

YUSUF MLELA ATWAA TUZO YA IJUMAA SEXIEST BACHELOR!

....Mlela akinyanyua juu tuzo yake mara baada ya kutuzwa

...akikabidhiwa na Mr. II 'Sugu'

Pamoja na tuzo, alipewa pia cheti maalum

Kanumba, ambaye ni mshindi wa mwaka 2007 naye alikuwepo kupokea cheti chake kwa kufikia fainali za mwaka huu

MC alikuwa Ben Kinyaiya...akiteta na 'best' wake Maimatha
Mdhamini Mkuu wa tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor na Ijumaa Sexiest Girl, Tippo Athuman ambaye ametoa offer kwa Mlela kufanya shopping ya nguo za thamani ya shilingi za bongo 500,000 katika maduka ya Zizzou fashions

..Mzee Zorro naye alikuwepo ku support vijana

...penye wengi hapakosi mengi

Mamaa Asha Baraka (kulia) akiwa na Dotnata ambao wametoa mchango mkubwa sana kufanikisha hafala hii fupi iliyofana ya kutoa tuzo

Fainali ya kumsaka kijana mtanashati wa gazeti la Ijumaa, ‘Ijumaa Sexiest Bachelor,’ usiku wa kuamkia leo ilifikia kilele chake, ambapo msanii chipukizi wa filamu hapa nchini, Yusuf Mlela, alitangazwa mshindi katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa TTC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, na kushereheshwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’.