Monday, December 21, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Sugu: Zimebaki saa 72 za maajabu Diamond
Mwana Hip Hop ‘Next Level’ Bongo, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ amebakiza siku 3 au saa 72 kuzindua albamu yake ya 10, ambayo inaundwa na mawe 10 ya adabu, ambayo muda ukifika, itakatiza kitaani kwa jina la Veto.

Mr. II ambaye anajulikana pia kwa jina la Sugu, wakati zamani aliitwa 2 Proud, ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, katika shoo ambayo inachukuliwa kama tambiko la Bongo Flava.

Albamu hiyo, Sugu ameiandaa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo.

Wana-Hip Hop wenye heshima Bongland kama Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’ kwa pamoja wameingiza vocal kwenye albamu hiyo.

“Nataka watu waone harakati zetu na jinsi tunavyoutetea muziki wetu, Bongo Flava haiwezi kufa, wanaobisha waje Diamond Jubilee”.
*****************

Zay B: Ugonjwa unaomsumbua wajulikana
Mtoto mwenye jinsia ya kike, mwenye rekodi ya kuwa wa kwanza kuingia studio na kufanya wimbo na kufunika, Zainabu Lipangile ‘Zay B,’ hali yake si shwari na mwili wake umedhoofu kwa kiasi kikubwa.

Ukikutana na Zay B kitaani, unastaajabu huku alama ya mshangao ikipanda kwenye ubongo, wakati huo huo swali “Kulikoni?” Likichukua nafasi hata kama sauti haitotoka.

Hapa juzi-kati, Zay B aliongea na Abby Cool & MC George over the weekend na kuiambia kuwa afya yake inadumaa kwa sababu ya kusumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo.

“Naumwa ndugu yangu, sina mawazo wala nini, kinachonisumbua ni vidonda vya tumbo. Vinanitesa kweli, najitahidi lakini wapi ndiyo maana napungua kiasi hiki,” alisema Zay B a.k.a Mwanadada Gaidi.

Zay B aliendelea kusema: “Hivi karibuni, nililazwa kwenye Hospitali ya Kansa Kliniki iliyopo Tabata, ingawa kwa sasa angalau najisikia nafuu.”

Kabla ya kauli hiyo ya Zay B, tayari wadau wenye hulka ya kishakunaku, walishaanza kunong’ona kuwa Mwanadada Gaidi anakonda kwa sababu ya mambo ya game kumuendea kinyumenyume mpaka hasikiki.
*************************



Nivea Amewajibika on bed na R. Kelly, Lil Wayne
Ni bandika bandu, akichorwa huyu kesho anapandishwa mwingine katika ‘segment’ ile ile inayohusu malavidavi. Ebwana Dah!

Mwanamuziki Nevea Nash ndiye anayepanda kitini na hapa inatajwa orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti ameshiriki nao yale mambo yetu ya faragha a.k.a sanaa ya kiutu uzima.

Mfalme wa R&B, Robert “R” Kelly ndiye anayetajwa wa kwanza kukukuruka na mrembo huyo, ingawa haisemwi ni lini alianza kudondoka naye on bed.

Rap mwenye fedha nyingi, Lil Wayne anaorodheshwa nambari mbili, kwamba alianza kuchetuka naye mwaka 2003 hadi mwaka huu.

Kati ya mwaka 2004 na 2007, Nivea alijimwaga kwa Terius kabla ya kuachana na kila mmoja kuangalia ustaarabu wake.

Jina lake kamili ni Nivea Hamilton, umri wake ni miaka 27, alizaliwa Machi 24, 1982, Atlanta, Georgia, Marekani.
*******************************

No comments: