Friday, December 18, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!


Sugu: Bado saa 144 za tambiko la Bogo Flava
Galacha wa Hip Hop nchini, Joseph Osmund Mbilinyi ‘Mr. II’ amebakiza siku sita au saa 144 kuzindua albamu yake ya 10, ambayo inaundwa na mawe 10 ya adabu na muda ukifika, itakatiza mtaani kwa jina la Veto.

Mr. II a.k.a Sugu ataitambulisha albamu hiyo Desemba 24, 2009 (Mkesha wa Krismasi), katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, katika shoo ambayo inachukuliwa kama tambiko la Bongo Flava, kwamba baada ya hapo muziki wa kizazi kipya utarudi kwenye chati yake.

Albamu hiyo, Sugu ameiandaa nchini Marekani, kwenye Studio ya S&S Records iliyopo Brooklyn chini ya maprodyuza, Stiggo na Puzo.

Wana-Hip Hop wenye heshima Bongland kama Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, John Simon ‘Johmakini’ na Ahmed Dolla ‘Balozi’ kwa pamoja wameingiza vocal kwenye albamu hiyo.

“Nataka watu waone harakati zetu na jinsi tunavyoutetea muziki wetu, Bongo Flava haiwezi kufa, wanaobisha waje Diamond Jubilee, waone jinsi tunavyoutambia muziki wetu kwenye Mkesha wa Krismasi,” alisema Sugu.

TCC: chang’ombe:washiriki wanasemaje kuhusu fainali?
Marlaw
“Mimi sijui niseme nini kwa sababu mpaka hapa nilipofikia naona mashabiki wangu wamefanyakazi kubwa sana, wamenipigia kura na ninaomba waendelee kunipigia mpaka mwisho mpaka kitakapoeleweka hiyo Jumapili ndani ya TCC Club Chang’ombe.

“Nani atashinda, siyo swali ambalo mimi naweza kulijibu, inaweza kuwa mimi au mwingine kwa sababu hiyo ndiyo maana ya shindano, lakini kila kitu kipo sawa, na zaidi nimejionea tofauti na ubora wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor, kwakweli linatuweka karibu na mashabiki.”

Hemed
“Kwangu kila kitu naona kinakwenda sawa kwenye shindano, mimi nafuatilia na naridhika na utaratibu mzima na jinsi mambo yanavyoendeshwa, lakini kubwa kabisa nawashukuru wasomaji kwa kunipigia kura na ninawaomba waendelee kufanya hivyo, pia waje TCC Club Chang’ombe hiyo Jumapili ili wanipe kampani.
“Suala la ushindi lipo wazi, naamini mimi ndiye mshindi mia kwa mia, hata hivyo bado nawataka wasomaji wanipigie kura zaidi ili kunisafishia njia yangu. Kusema ukweli Ijumaa Sexiest Bachelor linatupaisha, ni shindano bora zaidi hapa Bongo.”

Yusuf Mlela
“Nawaheshimu sana wapigakura kwa kunifikisha hapa nilipo, bila wao nadhani ningetolewa mapema. Kwa upande wa shindano, nafikiri hili lipo the best kwa mashindano yote ya kiume kwa sababu mbali na mshindi kupata zawadi, lakini linatusaidia kukua na kutuweka karibu zaidi na mashabiki wetu.

“Kuhusu shindano, bado nategemea wapigakura kwa sababu ni wao wenye nafasi ya kunifanya nishinde au la! Ila sina hofu kuwa nitashinda. Washindani wengine nawakubali, kwahiyo tukutane TCC Club Chang’ombe hiyo Jumapili tumalize ubishi.”

Kanumba
“Watu wanatakiwa kuhudhuria kwa wingi TCC Club ili wajionee mshindi. Ijumaa Sexiest Bachelor ni bonge la shindano, na wote tuliofika fainali, kila mmoja yupo vizuri na anaweza kushinda. Binafsi nawashukuru wasomaji kwa kunifikisha fainali.

“Ila tukienda mbele zaidi, kati ya wote walioingia fainali, mimi ndiye mkongwe kwa sababu Marlaw, Hemed na Yusuf ni vijana walionza kuvuma juzi, halafu pia ndiye ninayeshikilia taji hili, tangu niliposhinda mimi mwaka juzi, hajapatikana mwingine, kwahiyo nadhani nina kila sababu ya kushinda.”

Twanga kufunika
Kunako fainali hizo za Ijumaa Sexiest Bachelor zitakazochukua nafsi pana TCC Club, Chang’ombe, Dar es Salaam Jumapili ya keshokutwa, Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ndiyo itakayobeba dhamana yote ya burudani kwa kuhakikisha kila kitu kwa upande wao kinakwenda sawa ukizingatia kwamba ndiyo bendi inayotamba hivi sasa Bongo kupitia mastaa wake kama Chalz Baba, Kalala Junior, Salehe Kupaza, Chokoraa na wengine kibao. Kwa kifupi siyo ishu ya kukosa, kiingilio ni buku saba tu (7,000) kwa kila mtu, njoo umshuhudie mshindi laivu.

Compiled by mc george


No comments: